Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Wednesday, February 22, 2012

WEMA AFANYA KUFURU DUBAI

Na Mwandishi Wetu Maisha ya Wema Isaac Sepetu yamebadilika, sasa anaitwa pedeshee Sepetu kufuatia matukio yake ya hivi karibuni yanayohusisha matumizi makubwa ya fedha ambapo gumzo ni lile alilofanya kufuru katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), mjini Dubai.

SHOPPING YAGHARIMU ZAIDI YA SHILINGI MIL. 45
Habari zilizosambaa kwenye mitandao mingi ya burudani na kijamii ndani na nje ya Bongo mwishoni mwa wiki iliyopita, zilisema kuwa Wema siyo wa bei ndogo tena baada ya kumwaga mamilioni ya fedha kwa ajili ya shopping iliyodaiwa kugharimu dola za Kimarekani 40,000 (zaidi ya Sh. milioni 45 za madafu).
AFIKIA HOTELI YA NYOTA TANO
Katika habari hiyo, Wema aliyefikia katika hoteli ya nyota tano ya DXB mjini humo, alipiga picha akiwa kwenye moja ya maduka ya kistaa akinunua bidhaa za bei mbaya zikiwemo pafyumu, dhahabu, viatu na mazagazaga mengine.
MSHANGAO

“Inavyoonekana mwanadafada Wema siku hizi baada ya kuachana na Almasi (msanii Naseeb Abdul ‘Diamond’), amekuwa akijiachia na kufanya matanuzi ambayo duh! Amekuwa mtu wa shopping hapa home na sasa yuko zake Dubai kwa ajili ya shopping na matembezi kidogo,” ilisomeka sehemu ya habari hiyo ikiambatanishwa na picha.
 
MASWALI TATA
“Najaribu kutafakari ni kazi gani anayofanya Wema siku hizi ambayo imekuwa ikimlipa hadi anafuja fedha kiasi hiki? Maana zile pesa ni zaidi ya milioni 45, tena ni kama milioni sitini na pesa hivi...ni hela nyingi sana! Je, ni filamu tu au kuna kingine?” alihoji mmoja wa watu aliyesoma habari hiyo ambapo maswali ya sampuli hiyo yalikuwa mengi.

WEMA PEDESHEE?
Uchunguzi wa Risasi Mchanganyiko ulibaini kuwa, mbali na gari la Sh. milioni 35, aina ya Toyota Lexus Hybrid Harrier analosukuma mnyange huyo baada ya kusota na teksi kwa muda mrefu, pia amekuwa akituza wanamuziki wanapokuwa stejini katika kumbi mbalimbali za starehe jijini Dar es Salaam.
Katika utetezi wake, Wema aliliambia gazeti pacha na hili, Risasi Jumamosi kuwa, gari analoendesha alinunuliwa na familia yake kama zawadi baada ya kuachana na Diamond.
Achilia mbali gari na shopping za kufuru, pia Wema anaishi kwenye nyumba ya kifahari aliyopangisha maeneo ya Makumbusho Kijitonyama, Dar.

KUNA KIGOGO?
Nyuma ya matumizi ya kufuru ya fedha yanayofanywa na Wema, kuna madai mazito kuwa yupo mwanaume ambaye ni kigogo serikalini anayefanikisha yote hayo.
Kuhusu uwepo wa mwanaume anayefanya hayo yote, Wema aliwahi kujitetea kwa mwandishi wa habari hii kuwa, mambo hayo yote yanafanywa na mama yake mara tu baada ya kuachana na Diamond.

UTETEZI WA WEMA
“Kama watu wanasema nina bilionea, basi mama yangu atakuwa ndiyo bilionea wangu,” alisema Wema.

ANASEMAJE KUHUSU DUBAI?
Wema aliondoka Dar kuelekea Dubai kwa mapumziko ya msimu wa Valentine, hata hivyo, gazeti hili lilipomdadisi kama ameambatana na ‘mtu wake’ alichomoa.
Juhudi za kumpata Wema kusikia upande wake juu ya kufanya kufuru huko Dubai hazikuzaa matunda baada ya simu yake kutokuwa hewani kila ilipopigwa.

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.