Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Tuesday, February 28, 2012

DIWANI WA CCM IRINGA NA WENZAKE WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA MAUAJI

Diwani wa kata ya Maboga CCM Flugence Lutego (kulia ) akiwa na mtuhumiwa namba moja wa mauaji ya kijana Denis Kiluka ,kushoto ni mtuhumiwa namba moja Benison Mdongwe
Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya kijana Denis Kiluka akiwemo diwani wa kata ya Maboga Flugence Lutego (CCM) wakiingizwa mahakamani leo
Watuhumiwa watatu wa mauaji ya kijana Kiluka wakiwa na watuhumiwa wengine wakifikishwa mahakamani leo na askari polisi
Diwani wa kata ya Mabonga Flugence Lutego (CCM) akiwa amejifichwa kukwepa kamera za waandishi wa habari leo baada ya kusomewa shitaka la mauaji na kunyimwa dhamana
Mtuhumiwa namba tatu katika kesi hiyo ya mauaji Joel Kihwele akitoka mahabusu ya mahakama kwenda kupanda gari la mahabusu
Watuhumiwa wa mauaji wakifikishwa mahakamani leo
Diwani Lutego(kulia) na mtuhumiwa namba tatu wakipanda karandinga la polisi tayari kwa kwenda mahabusu mtuhumiwa namba moja wa kesi ya mauaji Bw.Benison Mdongwe akitoka mahabusu kwenda kupanda karandinga la polisi

DIWANI wa kata ya Maboga tarafa ya Kiponzero wilaya ya Iringa vijijini Flugence Lutego (41) na wananchi wake wawili wapandishwa kizimbani leo kwa tuhuma za mauaji ya mwendesha piki piki Denis Kiluka mkazi wa Isoka kata ya Mwangata katika manispaa ya Iringa .

Watuhumiwa hao walipandishwa kizimbani mbele ya hakimu mkazi wa mahakamani ya wilaya ya Iringa Mary Senapee leo majira ya saa 5.20 leo asubuhi na kusomewa shitaka hilo la mauwaji hukuwa wakitakiwa wasijibu lolote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo ya mauwaji.

Akisoma shitaka hilo mbele ya hakimu Senapee wakili wa serikali Lilian Ngilangwa alisema kuwa mtuhumiwa namba moja katika kesi hiyo ya mauaji kesi namba 8 ya mwaka 2012 ni Benisony Mdongwe (30) ,Flugence Lutego (41) na Joel KIhwele (39) ambaye ni mtuhumiwa namba tatu katika kesi hiyo.

Alisema kuwa watuhumiwa wote ni wakazi wa kijiji cha Makombwe kata ya Maboga tarafa ya Kiponzero wilaya ya Iringa vijijini na ni wakulima wa kijiji hicho ambao kwa pamoja wanatuhumiwa kumuua kijana Denis Kiluka siku ya Februari 12 mwaka huu katika kijiji hicho cha Makombwe Iringa vijijini.

Wakili huyo wa serikali Ngilangwa alisema kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo la mauwaji na hivyo kwa pamoja wanashitakiwa kwa kesi ya mauaji namba 8 ya mwaka 2012 kifungu cha 196 sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Hata hivyo baada ya kusomwa kwa shitaka hilo hakimu Senapee alisema kuwa kwa mujibu wa kifungu namba 148 cha sheria kesi hiyo haina dhamana kwa watuhumiwa na hivyo watuhumiwa wote watatu mbali ya kutotakiwa kujibu chochote kutokana na mahakamani hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo watakwenda mahabusu hadi kesi hiyo itakapotajwa tena machi 13 mwaka huu. 
 

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.