Na Mwandishi wetu
BAADHI ya wananchi wamesema utajiri wa Mchungaji Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ (pichani) unatisha.
Hivi karibuni, Lusekelo alisema kuwa mwaka uliopita pekee, alitumia shilingi milioni 380, kulipia vipindi vya runinga ili kuwafikia Watanzania.
Kutokana na hilo, wananchi wameliambia Uwazi kuwa Lusekelo ni tajiri mkubwa kutokana na kauli yake mwenyewe kwamba anatumia mamilioni kuendesha vipindi vya runinga.
Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita katika moja ya vipindi vyake, Lusekelo alisema fedha hizo zimemuwezesha kutoa neno kwa Watanzania wengi kupitia televisheni.
“Niwashukuru wote waliochangia kipindi cha Tutashinda. Hiki ni kipindi changu. Kuna wengine wanasema kwa nini jina la akaunti ni langu, nasema hiki ni kipindi changu na hizi fedha ni zangu siyo za kanisa,” alisema Mzee wa Upako.
Aliongeza kuwa hata akifa kipindi hicho kitakufa kwa kuwa ni chake lakini akasema Mungu huwa anaweka mbadala pindi anapoona anataka kumuondoa mtumishi wake duniani.
Mchungaji huyo wa Kanisa la GRC alisema, anawashukuru waumini wote wanaolichangia kanisa kwani awali lilijengwa likiwa na uwezo wa kuchukua watu 70 tu lakini sasa linabeba watu 5,000.
“Nilianza kazi hii ya kuhubiri neno la Mungu Iringa Stendi mwaka 1983. Nina miaka 29 katika kazi hii, japokuwa ukiniangalia utafikiri mimi bado ni kijana, nasema tushukuru na kujivunia hili.
“Samahani kwa kusema haya kuwa Kanisa la KKKT (Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania) lilianzishwa na Martin Luther King na linapewa ruzuku na serikali ya Ujerumani lakini GRC halisaidiwi na serikali, ni nguvu ya waumini, nawapongeza sana,” alisema Lusekelo.
Inasekana kuwa Lusekelo amefunguliwa na Mungu kwa kupewa uwezo wa kuombea watu na alianza kazi ya utumishi huo akiwa katika hali ya chini, akihutubia kwa kutembea kwa miguu mitaani lakini hivi sasa anatumia gari aina ya Range Rover Sport.
Inaelezwa kuwa wengi wanaamini huduma yake, ndiyo maana wakiambiwa wamchangie, huwa hawasiti, hivyo kumuwezesha kupata utajiri anaoutumia kuwafikia waumini.
No comments:
Post a Comment
Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.