Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Tuesday, February 28, 2012

CCM yarudi tena Arumeru



•  Mchuano kuwa baina ya mtoto wa Sumari, Sarakikya

na Happiness Mnale

KAMATI Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), imeshindwa kutegua kitendawili cha kumwidhinisha mgombea wa chama hicho katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki na sasa imeamua mchakato wa kura za maoni urudiwe baina ya wagombea wawili waliopata kura za juu.
Awali kulikuwepo na fununu za kuenguliwa kwa mtoto wa marehemu Jeremiah Sumari, Siyoi Sumari, ambaye aliongoza katika kura za maoni, kwa kile kilichodaiwa kuwa uraia wake una utata.
Katika mchakato wa awali jimboni Arumeru Mashariki, wagombea sita walijitokeza ambapo Siyoi aliongoza kwa kupata kura 361 akifuatiwa na William Sarakikya (259, Elirehema Kaaya (205), Elishilia Kaaya (176), Anthony Musani (22) na Rashankira Urio (11).
Hata hivyo, jana Kamati Kuu ya CCM (CC) ilibatilisha matokeo hayo na kuamua mchakato huo urudiwe upya jimboni humo Machi 1 na 2 mwaka huu, kwa kile kilichoelezwa kuwa hakuna mgombea aliyepata kura zaidi ya asilimia hamsini.
Na kwa mantiki hiyo, wagombea wawili waliopata kura za juu ni Siyoi Sumari na William Sarakikya ambao watamenyana katika duru hiyo ya pili ili kupata mgombea wa kupeperusha bendera ya CCM.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC), Itikadi na Unezi, Nape Nnauye, alisema kamati ya siasa itapitia kura kabla ya kutangaza jina la mgombea Machi 3.
Aidha Nape alisema kuwa watakaosimamia mchakato huo ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa, Naibu Katibu Mkuu, John Chiligati, na mjumbe wa baraza la CCM, Constansie Buhie.
Kuhusu tuhuma za uraia wa Sioi zilizokuwa zikitishia uteuzi wake, Nape alisema haukupatikana ushahidi wa kuthibitisha jambo hilo.
Alisema tuhuma hizo zinatokana na makundi ndani ya CCM na wanaosema hivyo hawajui utaratibu.
Aliongeza kuwa hata suala la kurudia kura za maoni halimo ndani ya katiba bali ni la kanuni za chama hicho.
“Hili jambo si jipya wala la ajabu ni la kawaida na ukikumbuka vizuri lilishatokea mwaka 1995 wakati hakuna mgombea kati ya watatu, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na David Msuya, ambaye alikuwa amepata kura zaidi ya nusu na kura zilirudiwa akapatikana mshindi ambaye alikuwa Mkapa,” alisema Nape.

Tanzania daima

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.