Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Wednesday, February 29, 2012

Dkt. Bilal Amaliza Ziara Iringa

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Iwawa baada ya kuzungumza nao wakati akimaliza ziara yake ya Wilaya ya Makete Mkoa wa Iringa jana Februari 28, 2012.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti cha kumiliki hisa katika Benki ya Wananchi (NJOCBA), Olive Luena, bada ya kuzindua rasmi benki hiyo iliyopo Wilaya ya Njombe mkoa wa Iringa jana Februari 28, 2012.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha SAO Hill, Nick Moore, hukusu ufanyaji kazi wa mashine mpya nay a kisasa ya kuchana mbao iliyofungwa katika kiwanda hicho, wakati alipofika kiwandani hapo jana Februari 28, 2012, kilichpo Wilaya ya Mafinga mkoa wa Iringa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya silaha ya jadi ya kabila la Wahehe (Mkuki) kutoka kwa Mjukuu wa Chifu Mkwawa, Ignas Muyinga, baada ya kumaliza kuzindua kituo cha afya na kuwahutubia wananchi wa Kijiji cha Lungemba, Wilaya ya Mafinga mkoa wa Iringa, jana Februari 28, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wananchi wa Kijiji cha Lungemba baada ya kuwahutubia wananchi hao, Wilaya ya Mafinga mkoa wa Iringa, jana Februari 28, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.