Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Saturday, February 25, 2012

BILAL AFUNGUA SOKO TUNDUMA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Soko la Tunduma lililofanyiwa ukarabati baada ya kuungua moto mwaka jana, wakati akianza rasmi ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Mbeya jana Februari 24, 2012. Kushoto ni Mkewe Mama Asha Bilal, (kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro na (kulia kwake) ni Mbunge wa Mbozi Magharibi David Silinde.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye eneo la Soko la Tunduma jana Februari 24, 2012, kwa ajili ya kuzindua soko hilo baada ya kukamilika kwa ukarabati wake kufuatia moto ulioteketeza soko hilo mwaka jana. Makamu wa Rais amewasili mkoani Mbeya jana kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Tunduma wakati alipofika eneo hilo kwa ajili ya kuzindua Soko la Tunduma baada ya kukamilika kwa ukarabati kufuatia soko hilo kuungua motoa mwaka jana. Picha Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.