Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Sunday, February 26, 2012

wanaume wanaume!! Chonde chonde jamani!!!!!!!

Habari yako dada Rose, natumaini wewe na familia yako ni wazima leo nakutumia hii mada kuhusu maisha ya rafiki yangu kwakweli mimi kama dada yake (wa hiari) inaniuma sana huyu dada anaishi na mwanaume wake ambaye wamekuwa pamoja wanakaribia mwaka sasa huyu dada yeye hana wazazi walishatangulia mbele ya haki, hana kaka wala dada yani alizaliwa peke yake.

Mara akakutana na huyu kaka kwakweli rafiki zake wote tulifurahia sana maana kwa mapenzi huyu mwanaume aliyokuwa anamuonyesha rafiki yetu tulimfurahia kwani amepata wa kumpenda wa kufidia nafasi ya wazazi wake japo hakuna mtu anayeweza kuifidia.

Mwaka wa pili huu sasa huyu dada kwa bahati nzuri amepata ujauzito, ambao kweli wote walifurahi sana lakini naona siku zinavyozidi kwenda huyu kaka hatumuelewi kabisa, ile mimba sasa inamiezi saba, huyu mwanaume kabadilika sana yani ukiachia vituko vyote mpaka anampiga!!!!!kweli unampiga mtu mwenye mimba ya miezi saba!!!!!

Juzi hapa ndio alivunja rekodi mwanaume kachelewa kurudi yule dada akawatuanamuuliza kwanini amechelewa kurudi basi yule kaka akaanza kumwambia hayakuhusu kwani huli, huvai, niache usiniulize kitendo cha yule dada kuongea tena tu basi alipigwa halafu yule mwanaume akaondoka.

Mara saa nane usiku huo nasikia simu inaita yule rafiki yangu analia anasema anaumwa tumbo na damu zinamtoka, nikamuuliza mwanaume yupo wapi akaniambia tu hayupo story ni ndefu anaomba tu nikamchukuwe nimpeleke hospital, basi mimi na mume wangu tukaenda kumchukuwa na kumpeleka hospital doctor akasema wampeleke kumpasua wamtoe mtoto maana kule kupigwa kulileta matatizo, basi na kwavile yule dada hakuwa na hela yoyote tukamlipia akafanyiwa operation na kujifungua mtoto wa kike.

Hakutaka kabisa tumueleze baba mtoto kama kajifungua, basi tukamhudumia mpaka aliporuhusiwa kutoka hospital sasa hakutaka kurudi nyumbani maana anasema alishateseka ya kutosha tukakaa naye kwetu cha kushangaza yule mwanaume wala hajamtafuta yule dada mwezi ukapita tukaamua sasa kumpangia chumba yule dada, tukampa na msichana wa kzai ili awe anamsaidia nasi tukawa tunamsaidia kwa hapa na pale japo mwenyewe anafanya kazi yake ya ususi hakosi kabisa hela ya kula.

Eti miezi miwili baadaye yule kaka akawa kama ameamka kutoka usingizini ndio anaanza kumtafuta yule dada kupitia sisi marafiki zake yani tena akija mpaka analia kama mtoto, anasema anampenda mkewe na kutaka japo amuone tu mwanaye, lakini kila akija mimi namwambia sijui alipo kwani mwenyewe alishakataa hataki kabisa kumuona yule kaka.

Machozi anayolia yule kaka kwakweli namuonea huruma sana japo alimfanyia rafiki yangu ubaya, roho inaniuma anavyoumia na ninashindwa kumsaidia kwani sitaki kuwa rafiki mnafiki kwa yule dada, jamani nimshauri vipi yule dada japo amuachie baba mtoto wake amuone japo mtoto? maana amekomaa kabisa hataki kuona sura yake.
 
http://rosemarymizizi.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.