Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Sunday, February 26, 2012

Mwanaume Apata Mimba Uingereza Azaa Mtoto wa Kiume


NewsImages/6252506.jpg
Thomas Beatie mwanaume wa kwanza duniani kupata ujauzito
Monday, February 13, 2012 11:20 PM
Kwa mara ya kwanza nchini Uingereza mwanaume amepata ujauzito na kujifungua mtoto wa kiume.
Mwanaume huyo ambaye jina lake limewekwa kapuni ametajwa kuwa mwanaume wa nne duniani kufanikiwa kupata mimba na baadae kujifungua mtoto.

Mwanaume huyo mkazi wa maeneo ya West Midlands alizaliwa kama mwanamke lakini baadae alibadilisha jinsia yake kuwa mwanaume pamoja na kufanya operesheni ya kuziondoa sehemu zake za siri za kike na kupandikizwa za kiume.

Hata hivyo mwanaume huyo aliomba mfuko wake wa uzazi usiondolewe na hivyo alibaki na uwezo wa kupata mimba kwa njia za kupandikiza ujauzito.

Mwanaume huyo alijifungua kwa njia ya operesheni mtoto wa kiume mwishoni mwa jana lakini taarifa za kujifungua kwake ndio kwanza zimetolewa wiki hii.

Mwanaume huyo amejiunga kwenye orodha ya wanaume wanne ambao wanajulikana kisheria kuwa ni wanaume baada ya kubadilisha jinsia zao kutoka kwenye jinsia za kike lakini baadae walifanikiwa kupata ujauzito kwa njia ya kupandikiza mimba.

Thomas Beatie wa Marekani ndiye aliyekuwa gumzo duniani mwaka 2008 baada ya kutangazwa kuwa mwanaume wa kwanza duniani kufanikiwa kupata ujauzito na baadae kujifungua mtoto wa kike.

Thomas hakuishia hapo ndani ya kipindi kichache baadae alifanikiwa kujifungua watoto wengine wawili wote wa kiume.

Wanawake wengine waliobadilisha jinsia zao kuwa wanaume na baadae kufanikiwa kupata ujauzito ni mmoja wa nchini Hispania na mwingine wa nchini Israel.


Nifahamishe.com  

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.