Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Monday, February 27, 2012

Nini maana ya Rastafari? na wanaamini nini?

Kuna watu wanampenda Bob Marley ama wanasema wanafuata nyayo au kuiga mfano wake, lakini ziko habari kwamba Bob Marley kabla hajafa alimpokea Bwana Yesu na kubatizwa kuwa muumini wa Orthodox na siyo Haile Selassie.

Alipokuwa katika mahojiano Askofu aliyembatiza Marley, Abuna Yesehaq wa kanisa la Ethiopia Orthodox, alisema Marley alikuwa mtoto wa Mungu tofauti na watu walivyomuona.

Aliendelea kusema "Ugonjwa wake wa kansa ulikuwa sababu kubwa ya yeye yeye kumpokea Bwana Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yake. Watu wengi walidhani alibatizwa kwa sababu alijua angekufa, lakini haikuwa hivyo, alibatizwa kwasababu hakuwa na msukumo kutoka kwa yeyote na alipobatizwa aliikumbatia familia yake na kulia kwa nusu saa."

Marley alibatizwa tarehe 4 Novemba 1980 na alifariki  21 May 1981 akiwa na miaka 36.

Tukiachana na habari ya Robert Nesta Marley au Bob Marley, Kuna dini ya marastafari na washirika wake tunao mitaani ambapo kwa asilimia kubwa ni vijana, Je dini hii ya marasta wanaamini nini? na rasta zinahusiana vipi na kuvuta bangi?

Marastafarian wanaabudu nini? Nini maana yake?

 Kuna vijana wengi wanaopenda au kuhusudu dini ya rastafarian na wengine kusema wanaabudu mungu anaitwa Haile Selassie. Nini maana ya haya? na yanahusiana vipi na kuvuta bangi? Je, wakifa wanaenda wapi?

Kwa marastafarian wanampenda Bob Marley au wanaosema wanafuata mfano wake, ziko habari Robert Nesta Marley au Bob Marley kabla hajafariki alimpokea Bwana Yesu na kubatizwa kuwa muumini wa Orthodox na kuachana na Haile Selassie.

Askofu aliyembatiza Abuna Yesehaq kutoka kanisa la Ethiopia Orthodox, alisema  ni Bob mtoto wa Mungu zaidi ya watu walivyomuona na alitamani kubatizwa tokea zamani lakini watu waliokuwa karibu naye walimvuta kwenye urasta.

Baada ya kubatizwa 4 Novemba 1980 askofu huyo alisema kwenye mahojiano yake "Marley ugonjwa wa kansa ndio ulimpelekea yeye kumpokea Bwana Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yake." 

Aliendelea kusema "Watu wengi walidhani Marley amebatizwa sababu alijua anakaribia kufa, lakini sivyo. Alifanya hivyo pasipo msukumo wa yeyote na alipobatizwa aliikumbatia familia yake wakalia pamoja karibu nusu saa"

Bob Marley alikufa na kansa mwaka 1981 akiwa na miaka 36 na Askofu Yesehaq ndiye aliyeongoza mazishi yake.

 Chanzo: Strictly Gospel

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.