maisha yangu ya ndoa yalikuwa mazuri na matamu sana kipindi cha mwanzo, mapenzi yalikuwa tele na ya moto lakini ikafika kipindi mume wangu akabadilika akawa kituko akawa mlevi mapenzi hana yani tunaweza kukaa hata miezi mitano hatujakutana kimwili akija nyumbani siku nyengine anatafuta ugomvi tu ili tupigane, na mara nyengine hata haachi hela ya matumizi nyumbani...
kwa muda mrefu nikawa namvumilia nikidhani atabadilika lakini wala hata wazo alikuwa hana, siku moja nikiwa kwenye hotel moja na rafiki zangu akaja mkaka mmoja mtanashati na rafiki zake wakajumuika nasi, huyu mwanaume akatokea kunipenda na kwamatatizo niliyonayo sikuona mbaya kama ningekubali kupenda na kupendwa tena...
nikamuadithia kila kitu kuhusu ndoa yangu, na akaahidi kunipa mapenzi kama sijawahi kupewa penzi tena, kwakweli huyu kijana kama alikuwa ameshushwa kutoka Mbinguni alinipa mapenzi mpaka nikamuona mume wangu kama kaka yangu.....
miezi ikapita siku moja nikagundua yakwamba nimepitisha siku zangu za hedhi, kwenda kupima nikagundua ya kwamba ni mjamzito na kwasababu hatukutani kimwili na mume wangu nikajuwa moja kwa moja ni wa mpenzi wangu wa nje, kwakuwa sikuweza kumuacha mume wangu ikabidi siku hiyo nilivyorudi nyumbani nimtomase mume wangu mpaka akajikuta juu ya kifua changu, na ndipo ikawa mwanzo wa kulea ujauzito ule.....
baada ya wiki mbili nikamwambia mume wangu kwamba mimi ni mjamzito alifurahi sana kwasababu hatukuwa na mtoto basi kwake ilikuwa furaha kubwa, moyoni mwangu nikijuwa sio sahihi kutokumwambia baba halisi wa mtoto huyu kwamba nina ujauzito wake....
kwakweli baada ya kubeba mimba mume wangu akabadilika zile tabia zake mbaya zote zikafutika akawa na mapenzi tele, yani wakati ukafika mpaka nikawa nashindwa kwenda kuonana na mpenzi wangu wa nje, nikaachana naye bila kujuwa nilikuwa nimebeba mtoto wake...
sasa mimba ina miezi saba, mume wangu anajisifu kila mara kwa ndugu na rafiki zake anatarajia mtoto, moyoni roho inanisuta sijamtendea baba wa mtoto huyu haki lakini nitakapousema ukweli mume wangu ataumia sana na sitaeleweka na jamii pamoja na ndugu zake.....
najuwa sijafanya mema itafanyaje sasa ama niseme tu ukweli?
kwa muda mrefu nikawa namvumilia nikidhani atabadilika lakini wala hata wazo alikuwa hana, siku moja nikiwa kwenye hotel moja na rafiki zangu akaja mkaka mmoja mtanashati na rafiki zake wakajumuika nasi, huyu mwanaume akatokea kunipenda na kwamatatizo niliyonayo sikuona mbaya kama ningekubali kupenda na kupendwa tena...
nikamuadithia kila kitu kuhusu ndoa yangu, na akaahidi kunipa mapenzi kama sijawahi kupewa penzi tena, kwakweli huyu kijana kama alikuwa ameshushwa kutoka Mbinguni alinipa mapenzi mpaka nikamuona mume wangu kama kaka yangu.....
miezi ikapita siku moja nikagundua yakwamba nimepitisha siku zangu za hedhi, kwenda kupima nikagundua ya kwamba ni mjamzito na kwasababu hatukutani kimwili na mume wangu nikajuwa moja kwa moja ni wa mpenzi wangu wa nje, kwakuwa sikuweza kumuacha mume wangu ikabidi siku hiyo nilivyorudi nyumbani nimtomase mume wangu mpaka akajikuta juu ya kifua changu, na ndipo ikawa mwanzo wa kulea ujauzito ule.....
baada ya wiki mbili nikamwambia mume wangu kwamba mimi ni mjamzito alifurahi sana kwasababu hatukuwa na mtoto basi kwake ilikuwa furaha kubwa, moyoni mwangu nikijuwa sio sahihi kutokumwambia baba halisi wa mtoto huyu kwamba nina ujauzito wake....
kwakweli baada ya kubeba mimba mume wangu akabadilika zile tabia zake mbaya zote zikafutika akawa na mapenzi tele, yani wakati ukafika mpaka nikawa nashindwa kwenda kuonana na mpenzi wangu wa nje, nikaachana naye bila kujuwa nilikuwa nimebeba mtoto wake...
sasa mimba ina miezi saba, mume wangu anajisifu kila mara kwa ndugu na rafiki zake anatarajia mtoto, moyoni roho inanisuta sijamtendea baba wa mtoto huyu haki lakini nitakapousema ukweli mume wangu ataumia sana na sitaeleweka na jamii pamoja na ndugu zake.....
najuwa sijafanya mema itafanyaje sasa ama niseme tu ukweli?
25 comments:
- AnonymousMar 24, 2011 09:28 AMwewe kwanza nikupo pole kwa yaliyokukuta kwani mwanadamu hujafa hujaumbika mimi ninachokushauri usijekutoa hiyo siri kwa mume wako yakuwa mimba uliyokuwa nayo sio yake usjaribu pls kwani maji yameshamwagika yazoeleki tena na tena kitanda hakizaii haramu na huyo aliyekupa ujauzito usimwabie ya kwamba mimba ni yake kwasababu anaweza kukudai mtotowake ikawa tabu kwako wewe zidisha mapenzi tu kwa mume wako aendelee kuwelewa yakuwa mimba ni yake na hii iwe siri yako usimwambie mtu mwingine kwani binadamu hana siri endelea kumwomba mungu akusaidie kwa kipindi hiki kigumu kwako na majaribuReply
- Duh kweli UKIMWI HAUWEZI KUISHA YAANI MTU ANATOKA NJE YA NDOA NA ANAACHIA MZIGO PEKU PEKU?? NADHANI TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA TU KAMA WANAWAKE WATA ELIMISHWA VYA KUTOSHA KUHUSU MAGONJWA SIO TU MTU ANA WASIWASI NA MIMBA TU UKIMWI JE?? MIMBA UTATOA NA UKIMWI??? AU NDIO UTAKIMBILIA LOLIONDO??Reply
KWAKWELI IWE FUNZO HATA KWA WANAWAKE WENGINE KAMA UNATATIZO NA MUME WAKO KWANINI MSIONGEE KULIKO KUTAFUTA WA NJE?? KWANI NI WAZI KUTOKA NJE YA NDOA SIO SULUHU ZAIDI YA KUJITAFUTIA MAGONJWA!! MIMI KAMA MWANAUME NIKIJUA HIO KITU NAKULIMA TALAKA UKAOLEWE MBELE HUFAI HATA BURE.NIMEONGEA KAMA MSHAURI (MWANAUME) NINAYE CHUKIA KUTOKA NJE YA NDOA KWASABABU ZISIZO MBELE WALA NYUMA.
SOMETIMES MNALAUMU WANAUME BURE ETI KAKUCHUNIA KUMBE MWENYEWE UMEJISAHAU UKO MCHAFU HATA HUMVUTII TENA AU UNATOA MAPENZI NUSU NUSU.HII IWE FUNZO KWA WANANDOA WOTE MTU KAMA UMEOA/MMEOANA LAZIMA MJUE KUTIMIZIANA HAJA ZENU NI LAZIMA UNLESS MMOJA WENU ANA TATIZO LA MSINGI KAMA KUUMWA NA MENGINE.KILA MTU ANA HISIA KAMA WEWE UNATOKA NJE NA YEYE ATATOKA COZ NAYEYE ANA HISIA KAMA WEWE.NA USIKUTE ALIKUA ANATOKA NJE AKIDHANI HUZAI KUMBE PENGINE TATIZO NI LAKE, ONA SASA ULIVYO NA MIMBA MAPENZI YAMERUDI.HII MADA IMENIBOA KAMA KUNA ALIYE UZIKA ANISAMEHE TU BURE MIE NACHUKIA SANA CHEATING KTK MAHUSIANO - AnonymousJul 30, 2011 12:16 PMwe ungejua mi nilivofurahi, wanaume mmezidi kutufanya sie tuna moyo wa chuma na nyie wanyama basi shughuli ndo hiyo dada lea mwanao angali tumboni na akija duniani kitanda hakizai haramu mwaya!Reply
- AnonymousAug 6, 2011 04:53 AMDada ulilofanya si la maana kubeba hiyo mimba ungejitahidi sana kama umeamua kutoka nje kutumia kinga kwa hali yoyote ile. Ila wanaume wana maudhi nao lakini kilichotakiwa hapo ilikuwa ni uvumilifu, busara, hekima na kumtafutia mahala ukaongea nae kujua tatizo ni nini si kwenda kinyume kama ulivyofanya. Hukumtendea haki Mungu wako na mume wako pia. Nashauri hiyo mimba usiitoe wewe zaa tu mengine yatafuata kila kitu kina mwanzo na mwisho wake. Acha tamaa ya haraka haraka. ujue kuwa "haraka haraka haina baraka kamwe"Reply
- AnonymousAug 6, 2011 09:42 AMI'm afraid to say that, NO WOMAN I WL TRUST IN THS WORLD EXCEPT MY MOM! I hate cheating and i cant cheatReply
- AnonymousAug 7, 2011 03:56 AMwewe dada inaonyesha uliikuwa mkorofi kwenye ndoa. nasema hivi kwa sababu mwanzoni umesema hiviReply
"tunaweza kukaa hata miezi mitano hatujakutana kimwili"
Baada ya kupata mimba ukfanya hivi
"kwakuwa sikuweza kumuacha mume wangu ikabidi siku hiyo nilivyorudi nyumbani nimtomase mume wangu mpaka akajikuta juu ya kifua changu..."
kwa kuzingatia maneno yako mwenyewe ni kuwa inawezekana ulikuwa unamnyima. ingekuwa yeye anakunyima, siku ulipomtomasa asingeitikia. ulishindwa nini kuongea naye?
nawaaasi wanabloggers wenzetu walio katika relationship na ndoa. tujitahidi kumtimizia mwenzenu raha za kimwili na inapotokea tatizo ongea. kutoka nje si suruhisho.
aidha, kama utaamua kutoka nje please please please tumia condom, narudia tumia condom!!! - AnonymousAug 24, 2011 03:56 AMficha ukweli ili kulinda ndoa yako. siri baki nayo rohoni. kumbuka kitanda hakizai haramuReply
- AnonymousAug 28, 2011 04:05 AMsiri pekee ndio itakayokunusuru, usimwambie mumeo wala huyo mwenye mimba maana utakuwa mgeni wa nani kama mumeo akikutimua? hautapokelewa kwenu wala kwa wakwe. POLE SANA SANA SANA SANAReply
- AnonymousSep 22, 2011 09:04 AMhuyu mwanamke ni mjinga tena ni mjinga hasa wewe, si ungeondoka kabisa kuliko kufanya hivyo? kosa sio kutoka nje, kosa ni kurudi ndani mjinga kweli wewe kumbe ndo maana kila siku utasikia wanawake wanapigwa hadi kufa.. sasa unafikiri akijua kama ana panga atakuacha? nani anataka hiyo fedheha, we unatakiwa UACHIKE TUU, tena unasema mlikutana hotelini tena mara kibao angekufumania ungekuta umeshatangazwa kwenye matangazo ya vifo mjinga mkubwa wewe labda nisikujue, ole wako, mi sikushauri lolote mjinga mkubwa, wanawake wengine ni kama mashetani unaweza kazaa paka hivi hivi unacheza na watu wewe unamdanganya mume wako hivyo... toka hapa.Reply
- AnonymousOct 25, 2011 03:22 AMHapana!! Sidhani kama kumtukana huyu dada ndio suluhisho,tena unathubutu kusema"SIKUSHAURI LOLOTE MJINGA MKUBWA'' duh ungekuwa MUNGU wewe duniani kungebaki mazingira tu!maana hata wanyama waharibifu ni wengi MUNGU angetufutilia mbali!Reply
Ni hivi dada yangu,maadam umetambua hilo ni kosa basi Neema ya MUNGU ipo juu yako,na kwa kosa ulilofanya ninahisi kilio chako sio mimba tu! Hakika hata ukimwi unao!mwanaume wa kukuona ghafla kakupenda!? ukamuachia mwili wako auchezee utakavyo,mmmmh wangapi anawaona kila siku eti ukajiamini umefika mahali sahihi?
USHAURI wangu,Fanya toba mbele za MUNGU ahidi kutokurudia tena!ukipata amani moyoni basi mpende mumeo na usimwambia chochote. Nenda kapime ukimwi na mumeo ijulikane huenda ukawa umeathirika na mumeo ni mzima hapo ndipo pakuweka wazi uovu wako na ujiandae kuachika ama huna ukimwi hiyo ni salama yako maana utakuwa umeomba Toba ya kweli kwa MUNGU(zab.65:2-3) maana utakuwa umemuepusha mtu asiyekuwa na hatiya,maana inaonyesha wazi mumeo alitaka mtoto na kukosa kwake ndo kukampa mawazo mpaka akawa mlevi,kweli pole kwa kuwa hukutumia hekima kuinusuru ndoa yako.MWANAMKE MPUMBAVU HUIBOMOA NYUMBA KWA MIKONO YAKE,neno la MUNGU ni kweli na uhakika.Zingatia hayo - AnonymousOct 27, 2011 07:33 AMPole sana kwa yaliyokukuta .wanaume ndio walivyo , alihisi wewe una tatizo na ndio maana aliamua kuwa mlevi na kuendelea na mambo yake maengine.huenda ya kutatafuta watoto .Kilichotakiwa ni kuwa mvumilivu tu .kutoka ndio ya ndoa yako sio suluhisho ,Umemkosea mumeo na kumuaibisha pia .Umemkosea Mungu pia. Ushauri we fikiria sasa namna ya kuishi maisha .haijalishi maisha yatakuwa magumu kwako kiasi gani .cha msingin uwe na amani.Andaa makao yako mapya uondoke hapo kwa mumeo .tafuta tu namna ya kumjulisha kwamba mtoto aliyebeba sio wako.ila usimwambie ana kwa ana.maana nauhakika ukijifungua ukambambikia mtoto amabaye sio wake itakukosesha amani maisha yako yote .na yeye and ndugu wakishtukia ndio soo zaidi.Muombe Mungu akusamemhe uendelee na maisha yako tu .baada unaweza kutafuta namna ya kumjulisha baba wa mtoto. Sidhani kama ni sahihi kuendelea kuishi na mume wako ukiwa na mimba ya mwanaume mwingineReply
- AnonymousOct 29, 2011 03:00 PMDada kwa kweli unatuweka mashakani sisi wanaume ambao hatujaoa, sasa kwa nini usingeongea vizuri na mme wako? alafu samahani kama nitakuwa nimewakwaza wanawake. kusema kweli mimi ni mwanaume na nimetembea na wanawake zaidi ya kumi na tano mpaka sasa, ni mooja tu ndo alinilazimisha nitumie kondom nae nadhani baada ya siku mbili tatu angeniachia peku peku, mimi toka nibarehe sijawahi kutiana peku, sasa huwa nawatania kama nataka kuingiza peku na wao wanaachia tu, hawakuulizi kondom ziko wapi? yaani huwa nashindwa kuelewa kama akili iko sawa sawa, tena wengine ni wanachuo na uelewa wanao, tena kuna mwanachuo mmoja akaniambia inamaana bado huniamini mpk tutumie kondom mpka leo? Sasa wewe dada kama ungetumia kondo yasingekukuta haya, kusema kweli wanawake mnakeraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, jitambueni sio mnapelekwa kama mazoba tu! wewe dada maji yameshamwagika wenzako wamepata somo sidhani kama watarudia ujinga kama wako, wewe subiri mpaka ujifungue ndo umwambie mme wako baada ya muda flan, ukimwambi sasa imekula kwako. Ni hayo tu.Reply
Ni mimi Izoo - AnonymousNov 1, 2011 01:48 PMBalaa kweli kweli haya usaliti mkubwa umefanya dada yangu au aunt yangu.Reply
- AnonymousNov 9, 2011 05:03 AMpole sista nafikiri upweke na kutokuongea kati yenu kumaliza mzizi wa matatizo yaliyowakabili kumepelekea yote hayo. Wote mna makosa hakuna aliyetaka kusimama katika nafasi yake kuinusuru ndoa yenu ndio maana yamefikia hayo. Sikulaumu sana kwani hayo ni mapito tu lea mtoto huyo na mumeo pia tafuta ushauri kwa wataalamu wa saikolojia pia watumishi wa MUNGU watakusaidia sana. Pia tubu hiyo dhambi isije ikakuumiza.Reply
- AnonymousNov 19, 2011 06:30 AMWAPUMBAVU KAMA HAWA WAKO WENGI SANA, NAWACHUKIA SANA WANAWAKE WA AINA HII....Reply
- AnonymousNov 27, 2011 12:37 PMkoma weee hata wanaume mbona wanazaa nje kwani wao hiyo haki kawapa nani mxxxxxxReply
- AnonymousNov 28, 2011 09:19 PMDada nakushauri ondoka bila kuaga kaanze maisha yako kimya kimya na Mungu wako atakusaidia , ukishahama mjulishe mumeo kuwa umekimbia kwa kuwa una mimba ambayo si yake hapo unaweza sasa kumtafuta yule aliyekupa hali hiyo kama atakuelewa vinginevyo hapo kwa mumeo subiri uje unyongweReply
- AnonymousDec 4, 2011 02:14 AMwewe mwanamke wewe unawezaji toka nnje ya ndoa na kufanya mapenzi bila zana? kiukweli hapo umelikorogaaaa kabisaaaaaa yani hakuna msada na huyo mumeo unafikiri atakaa hadi lini bila kujua kama sio mtoto wake?POLE SANAReply
- AnonymousDec 6, 2011 05:42 PMWANAWAKE NDIO WALIVYOO WANADANGANYIKA KIRAHISI SANA PLS ENYI WANAWAKE KUWENI WAVUMILIVU KATIKA NDOA ZENU KWA TABIA HIO HATUTAFIKA DADA MWOMBE MSAMAHA MMEOReply
- AnonymousJan 3, 2012 11:52 PMMie nimwanaume lakini ni vema ukausema ukweli japo utakubidi uondoke hapo home kwenu. kwani kwa kwakumficha huyo mmeo ni hatari sana atajua tu kama unamwamini Mungu basi tegemea kupata mtoto ambaye atafanana kweli kweli na baba yake mzazi. Hapo umechemka. Ubaya wote wa mumeo utaubeba wewe kwa asilimia zote. pole sana.Reply
- AnonymousJan 17, 2012 09:33 PMPole sana dada tunza siri yako usimwambie yeyote yule, hayo ni ya kawaida katika dunia hii.Reply
- AnonymousJan 24, 2012 07:33 PMnimeipenda hiyo kosa la kutoka nje ya ndoa ni kwa mwanamke tu ila mwanaume akitoka yeye ni rijali safi sana mbona sisi kina mama mnatuacha ndani mnaenda kuzaa nje ya ndoa na sisi tunavumilia na mtalea watoto haramu mpaka mbadilike siku zote siri ya mtoto ni wa nani anajua mamaReply
- JovinalJan 25, 2012 10:44 PMUpuuzi mtu huo, huyu demu alipaswqa kujiheshimu licha ya kutoka nje ya ndoa. Kwani angetumia kondomu raha asingepata? Kuna utafiti fulani wa Mpango wa Kudhibiti Ukimwi Tanzania unaoonyesha kuwa wanadoa hawapendi kutumia kondomu hata pale wanapokuwa nje ya ndoa zao. Ni funzo, tujifunze!Reply
Kwa kuwa hukuwa na maamuzi ya kutumia ama kutotumia kondomu umepata mimba na hatujui kuhusu magonjwa mengine.
Kutoka kwako nje hakujakusaidia ila kumeleta matatizo zaidi. POLE
Nina kesi ya jirani yangu ambaye mtoto wake wa kwanza kati ya watoto watatu hakuwa wa mume wake. Mume amekuja kugundua baada ya miaka kama kumi. Ni vurugu tupu ndani hakukaliki.
USHAURI
TRUTH WILL MAKE YOU FREE (Ukweli utakufanya uwe huru)
Ni ngumu sana, ila mweleze ukweli kwa kutumia wajumbe watu wazima anaowaheshimu huku na wewe ukijiandaa kuachika, maana kusema ukweli wanaume hatuna uwezo wa kuvumilia hilo
Huwezi kutoa mimba maana tayari anaijua, na zaidi katika hilo sikushauri japo dhambi ninazo, hiyo ni ni kuua.
Jua kuwa wapo wengi wenye matatizo kama hayo, si wewe peke yako.
Hata ukificha ipo siku tu atajua, ukizingatia ndiye mtoto wenu wa kwanza, ndugu zake lazima wajae kumwona na ndiyo wakute si damu yao patachimbika.
La mwisho upo uwezekano huyo mwanaume hana uwezo wa kumrutubisha mwanamke