Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Wednesday, February 29, 2012

MREMA NAYE AKATAA POSHO


Pamela Chilongola na Keneth Goliama
MWENYEKITI wa Chama Cha Tanzania Labour  Part (TLP ) Augustino Mrema amemtaka Spika wa Bunge, Anne Makinda kuwa  na uvumilivu na kiwango cha mshahara wa   wabunge wanachokipata.Akizungumza  na waandishi wa habari  ofisi kwake jana, Mrema alisema wabunge wanatakiwa kuogopa kutawaliwa na tamaa ya fedha katika kuongoza wananchi.

Mrema alisema wabunge hawahitaji kuwa mamilionea katika kuwasaidia wananchi bali kuna miradi mbalimbali kama mfuko wa jimbo na kufungua miradi ya maana katioka  kuinua uchumi wa wananchi.

“Ni kweli fedha  tunazolipwa hazitoshi lakini tunatakiwa kuvumilia na kuendelea kuongoza maana hata ukipewa Sh10 milioni  haziwezi kutosha iwapo mbunge hatakuwa na  matumizi ya mipango thabiti,” alisema.
Mrema alisema kinachoongelewa na Spika Makinda ni kweli lakini  mbunge anatakiwa kuweka bajeti katika  kuendesha jimbo lake.

Alisema  kama wabunge wanataka kuondoka kwa ajili ya kukosa posho na mishahara waende lakini kwa yeye  hawezi kuondoka  kutokana na kiwango hicho kumtosha sana.

 “Nimekaa zaidi ya miaka 20 bila kupata chochote, niliweza kuwasaidia wananchi wangu licha ya kujiuzulu uwaziri wangu, sasa kwanini leo niachie hata hiki kidogo siwezi kukiachia ng’oo! Haachii ngazi mtu hapa,” alisema mrema.
Alisema hakuna mbunge ambaye ataweza kuachia ngazi kwa ajili ya mshahara kuwa mdogo kutokana na kwamba kazi ya ubunge sio fedha bali ni kujituma kwa wananchi.

Marema alisema  Spika Makinda hatakiwi kulaumiwa kutokana na wabunge wachache waliongia bungeni kwa ajili ya kutafuta fedha  humfuata  na kumueleza matatizo yao.“Spika makinda ni  halalali kueleza kutokana yeye kuwa mama wa wabunge wote wa kupokea malalamiko na kuyafanyia kazi,” alisema.

Uteuzi wa mgombea Arumeru Wakatai huo huo chama cha TLP kimetangaza kusimamisha mgombea ubunge katika jimbo la Arumeru mashariki.

 Mrema alisema  chama kimempitisha Abraham Mhoza Chipaka kupeperusha Bendera ya TLP . Alisema kamati ya  halmashauri ya wilaya ya chama hicho ilimpitisha Mgombea huyo  kwa kuona nafaa kukiwakilisha chama.
“TLP tumejipanga kugombea Arumeru Mashariki tutaenda kugombea na sio kusindikiza kama wanavyofikilia”alisema na kuongeza:
 “Tumemsimamisha Abrahamu Chipaka ambaye ni mjasiliamali amepitishwa na kamati ya Halmashauri ya Wilaya Taifa”alisema Mrema. Mrema alisema anafurahishwa na migogoro inayoendelea ndani ya chama cha CUF na NCCR mageuzi kwa kile alichodai kuwa aliambiwa yeye ni dikteta na kufukuza viongozi katika chama alichokuwa akikiongoza.

“Uongozi ni mgumu wanatakiwa wajifunze kupitia vyama vingine wasibaki kushabikia na kuniona mimi ni dikteta kazi yangu ni kuwafukuza wanachama wenzangu,sasa kikowapi leo hii yamewageukia wao”alisema Mrema. Alisema suala la watu kumnyemelea ili kumuondoa uenyekiti hakubaliani nao kwa kuwa huyo anayetaka kuchukua nafasi hiyo anasifa yeyote kuwa mbunge.

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.