Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Saturday, February 25, 2012

Vodacom yakarabati Kituo cha Polisi Mto wa Mbu

Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba, akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa kituo cha Polisi Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha kilichokarabatiwa na Vodacom Foundation kwa mara ya kwanza tangia kijengwe mwaka 1967, kwa gharama ya sh. milioni 17. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye na kulia ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Nguvu Kamando.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba, akipongezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye katika hafla ya uzinduzi na makabidhiano ya kituo cha Polisi cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha, jumla ya sh. milioni 17 zilitumika katika kukarabati kituo hicho. Kulia ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Nguvu Kamando.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye kushoto akisalimiana na Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kaskazini, Nguvu Kamando kulia wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo cha Polisi cha Mto wa Mbu kilichokarabatiwa na Vodacom Foundation katikati ni Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa kampuni hiyo Mwamvita Makamba akishuhudia, jumla ya sh. milioni 17. zimetumika katika ukarabati wa kituo hicho kwa mara ya kwanza tangu kijengwe mwaka 1967.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC), Thobias Andengenye akipanda mti wa ukumbusho wa uzinduzi wa kituo cha polisi cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha baada ya kukarabatiwa na Vodacom Foundation kwa mara ya kwanza tangu kijengwe mwaka 1967 na kugharimu kiasi cha sh. milioni 17, wakishuhudia ni Mkuu wa Kituo hicho INSP Amilton Matagi, Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba, Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Nguvu Kamando.
Waandishi wa habari wakiwa kazini kama kawa wakati wa Makabidhiano rasmi ya Kituo cha Polisi cha Mto wa Mbu Wilaya ya Monduli mkoani Arusha kilichokarabatiwa kwa mara ya kwanza na Vodacom Foundation, tangu kujengwa kwake mwaka 1967, maboresho hayo yamegharimu kiasi cha sh. milioni 17.

Chanzo: www.thehabari.com

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.