Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Saturday, February 25, 2012

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI WAKISHIRIKIANA NA UBALOZI WA KUDUMU UMOJA WA MATAIFA WAMUAGA BALOZI SEFUE

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa New York, Dr Asha Migiro (kati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico, Mhe. Mwanaidi Maajar (kulia) na Kaimu Balozi Mhe Lilian Munanka wakiwa kwenye Hafla ya kumuaga Mhe. Balozi Ombeni Sefue iliyofanyikia Millenium UN Plaza Hotel New York , Nchini Marekani. Mhe. Sefue anarudi nyumbani kushika wadhifa mpya wa Katibu Mkuu Kiongozi.
Mhe. Balozi Ombeni Sefue (kushoto) akipiga picha ya pamoja na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Los Angeles, California, Abdul Majid (kulia) na Radia Dahal.
Mhe. Balozi Ombeni Sefue (wa pili toka kulia) akipiga picha ya pamoja na Mwambata wetu wa Jeshi Ubalozi wetu Nchini Marekani Brigedia Jenerali Maganga (kushoto) pamoja na Mama Maganga wakiwa pamoja na Mke wa Balozi wa kudumu wa Somalia Umoja wa Mataifa Dr. Elmi Ahmed Dualeh.
Kutoka kushoto ni Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar, Mhe. Kaimu Balozi Lilian Munanka, Mama Sefue, Naibu Katibu mkuu Umoja wa mataifa, New York, Dr Asha Migiro na Tully Malecela. Kutoka kushoto ni Given Malecela, Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar, Mama Sefue, Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa, New York, Dr. Asha Migiro na Tully Malecela. 
Wafanyakazi na maafisa wa Balozi za Tanzania, Washington, DC na New York wakipiga picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Mhe. Balozi Ombeni Sefuna Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar. (Kwa Ihsani ya Muhidini Issa Michuzi)

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.