Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Sunday, February 26, 2012

UMEWAHI FIKA KISIWA CHA ZANZIBAR?


Hapa utapata Malhaj,Mashekh na Maimamu wa baadae,kisiwa cha Zanzibar ni moja ya sehemu tulivu na yenye waungwana Duniani.
Kama ujionavyo waungwana walivyotulia  nyakati za jioni baada ya kumalizika kwa salat,hapa kuna wamiliki wa vyombo vya majini,wamiliki wa maduka makubwa Zanzibar na wengine wenye mashamba makubwa ya Karafuu.kama hujawahi kufika Zanzibar hujachelewa jaribu kwenda ukajionee mwenyewe.
Je unapajua hapa? sikumalizii utamu tushuke chini kwenye picha nyingine.

Ghorofa za Michenzani ambazo zilijengwa miaka ya nyuma kidogo bado mpaka leo zinaonekana hivii.
Ukifika Zanzibar kila utakapopishana na kina mama utakutana wamejihifadhi kwa kijitanda na shungi vichwani mwao.Usishangae ukishangawa kwa kutojistiri,hapo nawazungumzia kina mama na si kinababa.
Haya jaza mate mdomoni,maana ni madikodiko ya kila aina jioni ya Forodhani kisiwani Zanzibar.

Pweza,Ngisi,Mishikaki ya nyama ya ngo`mbe na mazagazaga ya kila aina ambayo ukikutana nayo pesa lazima zikutoke muungwana.
Hii tunaita Min Market ya mitaani,unapata kila aina ya mbogamboga za majani na mengineyo yanayohusu mambo ya jikoni/misosi kwa ujumla.
Ukiwa angani kisiwa cha Zanzibar unaweza kukiona hivi kwa ukaribu.

Magangaone

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.