Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Saturday, February 25, 2012

HAYA TENA KIJANA WETU KUFUNGA NDOA USIKU

Na Shakoor Jongo MWANAMUZIKI ‘sharobaro’, Naseeb Abdul ‘Diamond’ ameianika dhamira yake ya kutaka kuoa ndani ya siku chache zijazo huku akidai tukio hilo litafanyika usiku.
Diamond ambaye aliwahi kuwa mchumba wa msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu aliyasema hayo hivi karibuni akiwa nchini Afrika Kusini alipokuwa akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu juu ya maisha yake ya kimapenzi na kimuziki.
Alisema, mwaka huu hautaisha bila kufanya tukio hilo muhimu ambalo amekuwa akishauriwa na ndugu zake kulitekeleza haraka.

Anamuoa nani?
Huku kukiwa na minong’ono kuwa huenda msanii huyo akamuoa demu aliyewahi kudaiwa kutoka naye aitwaye Natasha au Miss Tanzania namba 2, 2006, Wema Sepetu, Diamond alisema:
“Najua wengi wanataka kumjua mchumba wangu ila itakuwa ni mapema mno kumtambulisha, wala siyo hao ambao watu wanawatajataja, tena mchumba wangu wa sasa siyo staa.”

Kwa nini ndoa usiku?
“Nimeamua tu, nitaifunga baada ya swala ya Inshah (saa mbili usiku). Ishu ya lini nitafanya hivyo nitawaambia baada ya kinyang’anyiro cha Tuzo za Kili kuisha maana sasa hivi nimeelekeza mawazo na nguvu zangu huko.
“Mchumba wangu nitamtambulisha siku ya fainali ya Kili Awards. Wadau wangu wanipe tu sapoti katika kipindi hiki ili hata pale nitakapokuwa naoa niwe na furaha ya kupata tuzo,” alisema Diamond.
Oktoba mwaka jana, Diamond alimvisha pete ya uchumba Wema lakini uchumba wao haukudumu kufuatia kutokea mazingira ya kutokuelewana kati yao.

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.