Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Saturday, February 25, 2012

MIAKA 50 YA BDP, JK AHUDHURIA NA KUPEWA HESHIMA KUBWA


Mgeni rasmi katika sherehe za miaka 50 ya chama tawala cha Botswana, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na Rais wa Botswana Luteni Jenerali Seretse Khama Ian Khama, wakimshangilia Rais wa Zamani wa Botswana Sir Kitumile Masire akifunua kitambaa kuweka bango la mahali ilipozaliwa BDP
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amekipongeza Chama Tawala cha Botswana, Botswana Democratic Party (BDP) kwa mafanikio yaliyopatikana nchini Botswana na watu wake.

Rais Kikwete ametoa pongezi hizo katika Sherehe za Kuadhimisha Miaka Hamsini (50) ya Chama cha BDP katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Botswana.
"Katika miaka hamsini ya uhai wake, BDP kimefanya mambo mengi mazuri nchini Botswana, katika ukanda huu na Afrika kwa ujumla na kimekuwa na historia nzuri ya kufanya mambo mengi mazuri ya kuvutia na kutolewa mfano barani kote" Rais amesema.

Rais Kikwete ametolea mfano wa Pato la ndani la Taifa la Botswana ambapo, wakati wa uhuru wa Botswana mwaka 1966, lilikuwa dola za kimarekani 70 tu, hadi kufikia dola za kimarekani 16,300 mwaka 2011.

"Haya ni mafanikio makubwa sana Barani Afrika" Rais amesema na kukipongeza kwa dhati Chama cha BDP ambacho kinatawala tangu uhuru wake.
Mapema akizungumza na wananchi Rais wa Botswana PM Gen. Seretse Khama Ian Khama ameeleza kuwa Tanzania imetoa mchango mkubwa na kuwa urafiki wa nchi mbili hizi ni wa kudumu.


Mgeni rasmi katika sherehe za miaka 50 ya chama tawala cha Botswana, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na Rais wa Botswana Luteni Jenerali Seretse Khama Ian Khama, Makamuw a rais wa Afrika Kusini Bw Kgalema Nontlanthe, na Marais Wastaafu wa Botswana Sir Ketumile Masire ( wa pili shoto) na Bw Festus Mogae, wakijiandaa kukata keki ya sherehe hizo katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Botswana leo February 25, 2012

"Tanzania imesimamia Uhuru, Haki na Ukweli barani Afrika" amesema na kueleza kuwa nchi yake itaendelea kusimamia na kuheshimu misingi hiyo.
Rais Khama pia amewakumbusha wanachama na wananchi wa Botswana kuwa umoja wao ndiyo ngao kubwa ya Chama cha BDP na kwamba chama hicho bado kiko imara kutokana na umoja wao huo na kinapania kuendeleza, kuuthamini na kuulinda Umoja wao.

Sherehe hizo zimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Bwana Wilson Mukama.

Rais Kikwete anatarajiwa kurejea Dar-es-Salaam kesho tarehe 25 Februari, 2012.
Mwisho.

Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais,
Gaborone, Botswana
24 Februari, 2012

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.