Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Thursday, February 23, 2012

Sisi ni Zadi ya Jinsi Tulivyo.


"Maisha yetu ya sasa ni kutokana na jinsi tulivyojiona mwanzo tulivyo na kuamini tulivyo mwanzo na tunaweza tena kuwa zaidi ya jinsi tulivyozoea kujiona tulivyo kwa kuamua kujiona tulivyo zaidi ya jinsi tunavyojiona sasa"                     Kuishi maisha duniani ni shule kubwa sana kuliko shule yoyote unayoijua, na muda mwingine mimi nadhani muumbaji wa dunia hii alituleta makusudi ili kuja kujifunza shule hii ya maisha. 





Na watu wengi ambao wamejikuta kuwa wanafaulu katika shule hii ndio hao tunaowaona wakiishi maisha ya raha mustarehe baada ya kuzipitia suluba na misukosuko ya kuishi na kufaulu mitihani ya maisha.

Vile vile wapo binadamu katika dunia hii wanaoishi maisha lakini hata siku moja hawajawahi kufaulu mtihani hata mmoja wa maisha, zaidi kila siku wakiona mitihani ikiwa migumu huamua kukimbia mitihani hiyo na kuamua kuishi maisha yasiyo jua ushindi wala kufeli.Watu wa aina hii, wanaweza kuwa wanatembea lakini ni marehemu tayari. Mwanafalsafa mmoja alisema binadamu wengi tunakufa mara nyingi sana kabla hatujaingia makaburini. Hivyo basi kukubali maisha madogo na kuishi bora liende ili mradi kumekucha ni sawa na kufa huku unatembea.

           Kuna muda ambao nilikuwa napitia historia ya maisha ya watu kadhaa wenye mafanikio makubwa Tanzania, akina Reginald Mengi,S.H.Amon, Bakhresa, Manji na hata baadhi ya viongozi wakubwa wa nchi yetu.Wapo baadhi niliofanikiwa kuwahoji na wengine nilifanya utafiti wangu kujua ukweli kuhusu historia ya maisha yao na hata historia ya watu tofauti wakubwa duniani. Baada ya kupata taarifa hizo nilikuja kujua ukweli kuwa maisha ya dunia hii ni shule kubwa sana, ambayo asilimia kubwa ya binadamu wameifeli, hata wale waliosoma katika shule za darasani na vyuo vikuu baadhi yao wengi wameifeli sana.


           Nikiwa nasoma chuo kikuu niliamini sana kuwa elimu yangu itakuwa ni jawabu tosha katika shule ya maisha nitakayoishi hapa duniani. Lakini nilishangaa sana katika shule hii ya maisha kuona kuwa hata wale ambao hawakusoma kama mimi wanaimudu shule hii ya maisha vizuri sana tena hata zaidi ya wale wenye elimu kubwa ya darasani  kwa mifumo yao na utaratibu wao na hapo ndipo nikajua kusoma ni rahisi sana kuliko kuimudu shule ya maisha, na ndiyo shule inayotakiwa kupewa nguvu nyingi ingawa hata kusoma ni muhimu pia.

Jambo kubwa nililoligundua na  ambalo ningependa kila Mtanzania alijue ni kuwa:Sisi si kama wanyama wengine duniani, sisi si kama mbuzi au ng’ombe au hata mbwa sisi ni jinsi tunavyojiona tulivyo na ni zaidi ya jinsi tulivyo, maisha yetu ya sasa ni kutokana na jinsi tulivyojiona mwanzo tulivyo na kuamini tulivyo mwanzo na tunaweza tena kuwa zaidi ya jinsi tulivyozoea kujiona tulivyo kwa kuamua kujiona tulivyo zaidi ya jinsi tunavyojiona sasa, na kuthubutu kufanya makubwa kulingana na jinsi tunavyojiona kuwa sisi ni zaidi ya jinsi tulivyo sasa.

Tunaweza kuamua kujiona zaidi ya jinsi tulivyo pasipo kuogopa  misukosuko yoyote ya maisha na hapo ni baada ya kuamua kujiendeleza na kujifunza kuwa sisi ni zaidi ya jinsi tulivyo.Si kwa kusoma darasani tu bali kwa kuthubutu kufanya mambo makubwa kulingana na jinsi tunavyojiona kuwa sisi ni zaidi ya jinsi tulivyo, kwani tukiamua kufanya jambo kwa kuangalia jinsi tulivyo sasa pasipo kuamini kuwa sisi ni zaidi ya jinsi tulivyo, twaweza kujikuta tukiamua kuchagua maisha ya chini sana na ya kimasikini kama wanyama wa  kufugwa, pasipokujua kuwa tunaweza kuwa vyovyote vile tutakavyo katika maisha yetu.Kwa mantiki hiyo ni makosa kuyakubali maisha na hali ya maisha iliyo chini huku tukitoa sababu za hayo yote kutokea.

Tuthubutu kuwa Tunavyotaka maishani, kimasomo, kimaisha, kisiasa, kifedha,Kibiashara, kiroho, kimahusiano, kiuongozi na hata kisanii kwani SISI ni zaidi ya jinsi tulivyo.

Geophrey Tenganamba, 0714477218 au gtlivemore@gmail.com
ASANTENI


No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.