Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Friday, February 17, 2012

SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN LAZINDUA KAMPENI YA KUPAMBANA NA UTAPIAMLO KWA WATOTO.

SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN LAZINDUA KAMPENI YA KUPAMBANA NA UTAPIAMLO KWA WATOTO.

Mwanaharakati wa Haki za Watoto na Afya zao Bi. Hoyce Temu akizungumza na wanahabari kuhusiana na kampeni ya kupambana na utapiamlo kwa watoto, ambapo amesema tatizo hilo ni kubwa sana hapa nchini na kuishauri serikali ielimisha jamii umuhimu wa kula chakula bora na pia kutoa ufafanuzi kuwa chakula bora ni kipi.
Dr. Ellen Otaru Okoedian akitoa mwongozo kwa wawakilishi wa mabaraza ya Wanafunzi kutoka wilaya za jiji la Dar es Salaam wakati Shirika la Save the Children lilipofanya uzinduzi wa taarifa ya Lishe leo jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wakiwa makundi kuandika mapendekezo wanayodhani yakifanyiwa kazi na Serikali yatasaidia kuhamaisha mpango wa kupambana na Utapiamlo kwa watoto.
Hoyce Temu katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Wabunge.
Makundi ya Wanafunzi hao katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Wabunge na waandaaji wa uzinduzi huo.
·MDAU WA HAKI ZA WATOTO HOYCE TEMU ASHAURI ELIMU YA LISHE ITOLEWE KWA WANANCHI.
Shirika la Save the Children Tanzania limesema licha ya kuwepo maendeleo, watoto wanne kati ya kumi wenye umri wa miaka isiyozidi mitano nchini Tanzania wamedumaa.
Katika muhtasari wa wa hali ya Tanzania inaonyesha asilimia 17 wameathirika sana na kila siku watoto 130 wanakufa kutokana na magonjwa yanayohusiana na utapiamlo.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa lengo la Milenia namba 4 linalotaka kupunguza theluthi mbili ya vifo vya watoto haliwezi kufikiwa bila kukabiliana na utapiamlo.
Akizungumza wakati wa hafla ya chakula baada ya kuzinduliwa kwa kampeni hiyo, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa Mh. Lediana Ng’ong’o ambaye ni mwanaharakati wa masuala ya lishe ameshauri serikali kuajiri wataalam wa lishe ikiwezekana katika kila wilaya nchini.
Naye Mdau wa Kuhamasisha Haki za Watoto na Afya zao Hoyce Temu aliyealikwa katika uzinduzi huo, amesema ni muhimu serikali ikatoa elimu ya lishe kwa wananchi, ili waweze kutambua umuhimu wa kula chakula bora na faida zake kimwili na kiakili.

FULL SHANGWE

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.