Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Tuesday, February 21, 2012

RC Bendera atinga lupiro kwa kazi hizi.....


Baadhi ya wanachama wa Chama cha Kuweka na Kukopa cha Walimu Wilaya ya Ulanga ( Ulanga Walimu Saccos) wakiomba dua kabla ya kuanza kwa
mkutano wao wa kumi wa Chama hicho uliofanyika Kata ya Lupiro, Wilayani humo, kabla ya kufunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( hayupo pichani) juzi Wilayani humo.Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( wa kwanza kulia mstari wa mbele) akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa Watendaji wa Serikali
ya Kata ya Mtimbira, Wilaya ya Ulanga, Mkoa wa Morogoro, juzi, alipotembelea kuona shughuli za ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Sekondari ya Mtimbira , kabla ya kufikia Machi 30, mwaka huu ambapo wanafunzi wote waliofaulu na kukosa nafasi kutakiwa kuanza masomo yao

.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kushoto) akikata utepe kuzindua gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T 620 AQR lililonunuliwa na Chama cha Kuweka na Kukopa cha Walimu Wilaya ya Ulanga ( Ulanga Walimu Saccos) hivi karibuni katika eneo la Lupiro , Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro , kama mradi wa kusomba mpungakutoka kwa wakulima na kufikisha kwenye mashine ya kisasa ya kumenya mpunga na kutenganisha mchele katika madaraja , mali ya Saccos hiyo.
Source:John Nditi wa habarileo

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.