Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Tuesday, February 21, 2012

Kaka Zitto na mkonge wake Tanga akabeba mkonge wa watu

Mbunge wa Kigoma Kaskazini(CHADEMA)Zitto kabwe amekuwa Tanga kwa ziara yake ya kichama na kubwa kuangalia zao la mkonge. Ana kila sababu ingawa hoja yake haikusikilizwa bunge la kumi mkutano wa sita.
Hoja yake ni kubwa juu ya haja ya kukamia kurejesha dhahabu hii ya tanzania iliyotoweka.
Mwaka 1964 Mkonge ulichangia 65% ya mauzo yaTanzania nje, mwaka 2010 Mkonge umechagnia 0.1% ya mauzo nje ambapo ni takribani dola za kimarekani 11 milioni pekee zilizoingizwa na zao hili.
Mbunge huyo alisema Hali inapaswa kubadilishwa kwani Mkonge una faida nyingi sana na bei yake katika soko la Dunia inazidi kupanda siku hadi siku.

Aliitazama dhahabu hii ya shambani kwa midadi mikubwa

Akiwa shambani alielezea hisia zake kama mwalimu anavyofanya kwa wale wanaomsikiliza.

Alipotoka shamba alienda kuzungumza na wananchi na alihutubia kwa namna ile ile anayoifanya yaani kwa msisitizo.

Alipomaliza mkutano watu walishangilia kwa staili hii ya kumbeba juu kwa juu.

Chanzo: Lukwangule entertainment

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.