Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Friday, February 17, 2012

Nitamsaidia Rias Kwa Uwezo wangu Wote- Sefue

 Mhe. Ombeni Sefue Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akizungumza na watanzania hawapo pichani wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyoandaliwa na  Jumuiya ya Watanzania waishiio Jijini NewYork na Vitongoji vyake, kushoto kwake ni Mwenyekti wa Jumuia Bw. Hajji na kulia na Katibu, Bw. Shaban


 Mhe.  Balozi akiwa na  Mke wake Bibi Anita Sefue( aliyeshika zawadi) ambayo  Jumuiya ya Watanzania walimkabidhi  Balozi kama kumbukumbu ya kuwa Mlezi wa Jumuiya yao, wengine katika picha ni viongozi wa jumuiya hiyo.
Mhe. Balozi Ombeni Sefue, akiwa na Mke wake Bibi Anita Sefue katika picha ya pamoja na sehemu ya watanzania waliohudhuria hafla hiyo


Na Mwandishi Maalum

New York

Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Ombeni Sefue amesema,amejipanga vema kumsaidia Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Serikali kwa ujumla kupitia wadhifa wake mpya wa Ukatibu Mkuu Kiongozi “Ninatambua dhamana hii ni kubwa, nzito na yenye changamoto nyingi,lakini nimejipanga kutumia uwezo wangu , maarifa yangu na ujuzi wangu wote kumsaidia Mhe, Rais na zinazoambatana na dhamana hiyo”.
Balozi Ombeni Sefue, ameyasema hayo kumpongeza kwa wadhifa wake huo mpya, hafla Watanzania waishio jijini New York na vitongoji vyake. Katika hafla hiyo iliyofanyika siku ya alhamisi na kuhudhuriwa pia na Mke wa Balozi,Bibi. Anita Sefue, amejipanga vema katika jukumu lake hilo jipya. Amewashukuru kwa kutenga muda wao kuagana naye na vilevile kumpongeza na kwamba ameguswa sana na tukio hilo. Katika mazungumzo yake na watanzania hao, Balozi Sefue, amesisitiza umuhimu kwa wao, kuzidumisha na kuziendeleza sifa ambazo zimeifanya Tanzania kuwa moja ya kati nchi zinazoheshimika Barani Afrika.Akazitaja misingi ya dini, rangi, kabila au jinsia “Watanzania tunaheshimika sana, tunaheshimika kwa sababu tumeweza kuendeleza na kudumisha mambo makuu muhimu ambayo ni utamaduni wetu wa kupendana,kuheshimiana, kutobaguana kwa misingi ya dini, kabila, rangi au jinsia, wito wangu ninapoagana nanyi ni kwamba muyaendeleze haya hasa nyie akasema Balozi Sefue.

Balozi Sefue licha ya kuwahakikishia watanzania hao kwamba sifa hizo kuwa ni umoja, mshikamano, upendo na kutobaguana kwa Na kusisitiza kwamba, licha ya kuwa wao sasa wanaishi na kuendesha shughuli
zao nchini Marekani. Lakini nyumbani kwao kwa asili ni Tanzania, na kwa sababu hiyo wanaowajibu pia kuwafundisha mambo hayo watoto wao, ikiwa ni pamoja na kuwarithisha mila na tamaduni za mtanzania na historia nzuri wanakotoka.Akisisitiza umuhimu wa kusaidiana, Balozi Sefue amesema watanzania wataweza
kusaidiana pale tu watakapokuwa na Jumuiya inayowaunganisha.Na kwa sababu hiyo akawataka kuienzi na kuendelea kuiimarisha Jumuiya yao ambayo yeyé, licha ya kuwa mlezi wao lakini aliwasaidia sana yaliyopelekea kuanzishwa kwa Jumuiya ya Watanzania New York na vitongoji yake. Akasema ni kwa kupitia Jumuiya yao ambayo viongozi wake wamepatikana kwa uchaguzi wakidemokrasia. kwamba ndipo mahali ambapo wanaweza kubadilishana mawazo ya namna gani ya kusaidiana wao kwa wao lakini pia kuwasaidia ndugu na jamaa zao waliowaacha nyumbani (Tanzania) na Taifa kwa ujumla. “ Niwapongenze na kuwashukuru kwa kukubaliana nami pale nilipowapatia ushauri wa kuunda Jumuiya yenu, ninashukuru kwamba tangu kuasisiwa kwake mmekuwa mkiendelea vizuri.
Kwa upande wao na wakizungumza kwa niaba ya watanzania wenzao, Mwenyekiti wa Jumiya hiyo Bw. Hajji na Katibu wake Bw. Shaban Musemba, wamemhakikisha Balozi Sefue kwamba kama sehemu ya kuenzi mchango wake uliotukuka, watahakikisha Jumuiya yao haifi.Wakasema katika kipindi kifupi ambacho Balozi amekuwa Mlezi wa Jumuia hiyo, wamejifunza mengi kutoka kwake, na kwamba wanasikitika watakosa mchango wake wa mawazo, ushauri na mwongozo. Lakini wanamtakia kila la kheri katika nafasi yake hiyo mpya ya kumsaidia Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.