Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Friday, February 17, 2012

Heche Wa CHADEMA Aonekana Kimataifa Zaidi



BARAZA LA VIJANA LA CHADEMA (BAVICHA)
HSE NO 170, UFIPA STREET, KINONDONI, P.O.BOX 31191, Dar es salaam.Tel/Fax, (022)2668866, E-
mail:info@chadema.or.tz, Website: www.chadema.or.tz

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UTEUZI WA MWENYEKITI WA BAVICHA KUWA MJUMBE WA
BODI YA INTERNATIONAL YOUNG DEMOCRAT UNION (IYDU)

Umoja wa Vijana wa Vyama vya Mrengo wa Kati Duniani (International
Young Democrat Union, IYDU) ulifanya mkutano wake mkuu nchini Australia
uliokutanisha vijana zaidi 120 kutoka nchi mbalimbali kuanzia tarehe 8- 14 Jan
2012 ambapo BAVICHA kama mwanachama wa umoja huu iliwakilishwa na
katibu Mkuu wake Deogratias Siale.

Mkutano huu pamoja na mambo mengine ulikuwa na agenda ya uchaguzi wa
viongozi kwa nafasi za mwenyekiti, naibu mwenyekiti, makamu wenyeviti 10 na
mweka hazina.

Katika uchaguzi huo, Bara la Africa lilikuwa na wagombea wawili katika nafasi ya
makamu mwenyekiti ambao ni Charles Owerdu kutoka Ghana na John Heche,
Mwenyekiti wa BAVICHA aliyependekezwa kuwania nafasi hiyo na nchi za
Ufaransa, Ugiriki na Ujerumani.

Demokrasia ilichukua mkondo wake ambapo wagombea wote wawili kutoka
Afrika hawakupata kura za kutosha kushinda nafasi hiyo ambapo makamu
wote 10 walitoka nchi za Ulaya, Amerika na Amerika ya Kusini na Bara la Afrika
lilikosa mwakilishi katika bodi ya uongozi wa IYDU.

Hivyo basi, bodi mpya ya IYDU iliyoketi jijini Sydney imemteua John Heche,
mwenyekiti wa BAVICHA kuwa mjumbe mshiriki wa bodi ya IYDU ambapo
atakuwa akisimamia masuala ya Afrika. Pia bodi hiyo imemteua Mercy Gakuya

wa chama cha DP cha Kenya kushirikiana na Heche katika kusimamia mambo
ya Afrika ambao kwa pamoja watakuwa wakihudhuria vikao vyote vya bodi hiyo
kwa mwaka mzima.

Hii ni fursa muhimu kwa BAVICHA na vijana wote wa Tanzania wanaohitaji
mabadiliko na uhuru wa kweli kwani pamoja na mambo mengine itasaidia
kuendelea kupata uzoefu, ujuzi na maarifa ya kuendesha mapambano ya kudai
haki.

Uteuzi huu unaendelea kuthibitisha kuwa Chadema siku zote kimekuwa kikipika
na kutoa viongozi, si tu wanaoaminika na umma wa watanzania peke yake bali
pia jumuiya za kimataifa na ulimwengu kwa ujumla.

Pia BAVICHA inapenda kutumia fursa hii kurekebisha kauli iliyotolewa na gazeti
moja la kila siku hapa nchini kuwa BAVICHA ilikwenda Sydney kuomba misaada.

Taarifa hiyo ilipotosha maudhui ya safari hii kwani kama mwanachama
BAVICHA ilihudhuria mkutano huo na ilichofanya ni kuripoti hali halisi ya kisiasa
inavyoendela hapa nchini kama walivyofanya wengine kwa nchi zao ili pia
kuwapa fursa wajumbe wengine wa mkutano huo kujifunza jinsi ya kuendesha
siasa kwa kua moja ya malengo ya mkutano huo ni kubadilishana uzoefu katika
mambo haya hususani kwa vijana.

Aidha, ni imani ya BAVICHA kuwa matatizo ya nchi hii kamwe hayawezi
kutatuliwa kwa misaada kutoka nje ya nchi. Tunaamini kuwa matatizo ya
watanzania yatatatuliwa na watanzania wenyewe kupitia viongozi bora wenye
maono na malengo thabiti ya kizalendo pasi kutegemea wageni na kama wageni
hawa wataona haja ya kusaidia basi watafanya hivyo kwa kuunga mkono tuu
juhudi hizi pasi kupigiwa magoti, utamaduni ambao umekua ukiendekezwa na
serikali ya Chama Cha Mapinduzi ambao unaishushia hadhi nchi yetu.

BAVICHA na Chadema kwa ujumla haitakaa hata siku moja kuabudu misaada ya
nje ili kutatua matatizo ya watanzania.

Imetolewa leo tarehe 16/02/2012, Dar es salaam na;
Deogratias Siale
Katibu Mkuu BAVICHA Taifa

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.