Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CDM) kwa mara nyingine tena kinakubali kuwaachia CCM jimbo la Arumeru katika uchaguzi mdogo unaotegemea kufanyika mapema mwezi wa nne mwaka huu 2012.Ni nakila sababu ya kukili kuwa CCM ni chama kilichopoteza mvuto sana na kunahaja ya chama pinzani kushika Usukani wa Kuiendeleza Tanzania yetu,Lakini cha kushangaza Chama tunachotegemea kuwa ndicho mkombozi wetu kwa siku za usoni hakipo tayari kupokea usukani toka kwa CCM.
Kwanini Nasema hivi ndugu watanzania wenzangu...?Naomba kuoonesha utaratibu mbovu na ukosefu wa umakini wa Viongozi wa CDM katika Chaguzi tatu (3) ndogo za Ubunge katika jimbo la IGUNGA,UZINI na sasa ARUMERU.Katika chaguzi hizi za ubunge ni wazi CHADEMA waliamua na wameamua kuichia CCM kutokana na namana operasheni za kampeni zinavyo endeshwa na aina ya watu wanaopewa kuendesha Operasheni za kampeni katika majimbo hayoi matatu tofauti.
1.UCHAGUZI WA IGUNGA
OPERASHENI KAMANDA wa kujenga chama na kampeni alikuwa ni MWITA MWIKWABE WAITARA ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa sera na utafiti pale makao makuu,Naomba kuonesha aina ya mtu huyu na jukumu alilokuwa amepewa la kuwa operasheni kamanda huko igunga ili hali kisiasa ni political failure;
WAITARA; Kwanza kabisa mwaka 2008 aliahamia CDM akitokea CCM huko Mwanza alikokuwa katibu wa chama cha Mapinduzi, Mwaka 2010 mwita WAITARA alishinda katika kura za maoni katika uchaguzi mkuu wa kugombea jimbo la TARIME mwaka 2010..
Ikumbukwe tarime ilikuwa ni ngome ya CHADEMA na hata Halmashauri ilikuwa chini ya CDM kuanzia kipindi cha CHACHA ZAKAYO WANGWE na baadaye baada ya kifo cha WANGWE jimbo likachukuliwa tena na CDM chini ya Mh.MWERA...lakini katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 CDM walipoteza jimbo pamoja na Halmashauri kupitia kwa huyu MWITA WAITARA...mwita alishindwa kwa kishindo na Mh.NYAMBARI MALIBA NYANGWINE wa CCM.
Huyo huyo Political failure aliyetupotezea jimbo la TARIME akapewa kuwa operasheni kamanda wa Jimbo la Igunga katika Uchaguzi mdogo wa..kama alishindwa kujisimamia yeye katika uchaguzi mkuu pale Tarime ngome iliyosheheni bendera za chama kila kona,akina wangwe alilijenga jimbo kichama kupita maelezo.Nadhani matokeo tuliyaona ya Igunga.!!!!(mtasema mbona tulipata kura nyingi elfu 23,ndugu zangu part 2 itaeleza hilo ila sio kwa sababu ya WAITARA).
2. UCHAGUZI WA UZINI-ZANZIBAR
Operasheni kamanda mwenye dhamana ya kuhakikisha chama kinajengeka na wanachama wanaongezeka, alipewa BENSON KIGAILA MASALAMAKALI SINGO..Huyu ni Mkurugenzi wa Oganizesheni na mafunzo pale Makao makuu.Kisiasa huyu jama amegombea ubunge mara 3(tatu) jimbo la KIKABWE-DODOMA..
kwa mara zote 3 alishindwa kwa kishindo na katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 alitupwa mbali kabisa na Mh.SIMBA CHAWENE(CCM).Mwaka 2009 BENSON aligombea uenyekiti wa CHADEMA DODOMA akashindwa kwa kishindo.
Huyo huyo political failure mwaka 2012 anapewa operasheni kamanda jimbo la UZINI...nadhani kila mtu anajua kuwa CHADEMA wameshindwa kwa kishindo.
3.UCHAGUZI WA ARUMERU
Operasheni kamanda wa kueneza, kujenga na kukampeni chama cha CHADEMA hilo jukumu kapewa JOHN MREMA..
Huyu ni mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri wa CHADEMA pale makao makuu..(usihoji inakuwaje anapewa wadhifa huo wakati JOHN MREMA hajawahi kuwa mbunge wala diwani wa chama sehemu yoyote ile katika nchi hii)
Kisiasa huyu MREMA mwaka 2010 katika uchaguzi mkuu alikwenda kugombea ubunge jimbo la VUNJO kule kwa MH.LYATONGA mrema wa TLP...Katika uchaguzi ule JONH MREMA alikuwa wa 3 (tatu) alipata kura 2000(elfu mbili) dhidi ya kura 36000 (elfu therasini na sita )alizopata Lyatonga Mrema.
Leo hii huyohuyo Political failure ndiyo amepewa dhamana ya kuendesha operasheni ya uchaguzi pale Arumeru..Je tutegemee nini toka kwa huyu JOHN MREMA kama sio yaleyale ya Uzini Na Igunga!
!Licha ya Arumeru kuwa karibu na arusha(Ngome ya Chadema) lakini hii haita saidia kitu endapo watu wanaopewa majuku makubwa ya kuimarisha chama wanakuwa ni watu wa aina hiii:
NB: Hawa wote wanateuliwa na sekretarieti ya CHADEMA makao makuu chini ya Dr. WILBROAD PETER SLAA. Umakini wa Dr.Slaa katika hili upo wapi? WAKO WAPI VIJANA HAWA WANAOKITUMIKIA CHAMA KWA NGUVU ZAO ZOTE?
1. JOHN HECHE - Mwenyekiti Bavicha
2. LAMECK - Aligombea mtela na alipata kura nyingi sana,na amekijenga chama pale Mtela kupita maeelezo.
3. DICKSON NG'ILLY - Aligombea ubunge TEMEKE...nadhani wengi mnamkumbuka ile siku pale Mwembe Yanga.
4. MTELA ALAMU MWAMPAMBA-Aligombea ubunge Mbozi Mashariki jimbo changa lisilo kuwa na Bendera hata moja ya CHADEMA lakini alipata Kura 32,000 (elfu therathini na mbili) dhidi ya kura 36,000 (elfu therathini na sita alizopata G. Zambi wa CCM).
5. ADAM CHAGULANI - Diwani wa kata ya Igoma Mwanza.
6. GREYSON NYAKARUNGU - Kamanda mpambanaji toka Serengeti
7. KASHINJE MASANJA - Kamanda mpambanaji toka Shinyanga Mjini
8. MASHUVE - Korogwe Tanga
9. BEN SAANANE - Kilimanjaro
10. BURTON GWAKISA - Mbeya mjini (UDSM)
Hawa nilio wataja ni baadhi tu ya vijana shupavu na wakomavu kisiasa ambao wamekuwa bega kwa bega katika harakati zote za kujenga chama, kampeni mbalimbali, mikutano mbalimbali wamekuwa wakikitumikia chama kwa moyo wa halii ya juu sana.
Ni wazi CHADEMA wamekubali Kushindwa ARUMERU.
Maelezo haya ni ukweli na uhalisia wa mambo....tunahitaji CHADEMA imara na yenye hadhi ya kuiondoa CCM madarakani.
Last edited by TUNTEMEKE; Yesterday at 12:43. Reason: ERROS
jamiiforums.com
No comments:
Post a Comment
Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.