Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Wednesday, February 22, 2012

NBC KUDHAMINI GOFU LA WANAWAKE


Maofisa wa NBC pamoja na wa Kitengo cha Gofu ya Wanawake cha Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam wakipiga picha ya pamoja katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo

Nahodha wa Kitengo cha Gofu ya Wanawake cha Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam, Vivienne Mwaulambo (kushoto) akizungumza kabla ya kupokea msaada msaada huo kutoka benki ya NBC. Katikati ni Meneja Udhamini na Matukio wa NBC, Bi. Rachel Remona Kimambo na kulia ni Katibu wa kitengo, Joyce Svarva.

Meneja Udhamini na Matukio wa NBC, Bi. Rachel Remona Kimambo ( wa
pili kushoto) akikabidhi mfani wa hundi ya shs milioni kwa Nahodha wa Kitengo cha Gofu ya Wanawake cha Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam,Vivienne Mwaulambo kusaidia mashindano yao yanayotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo katika klabu hiyo jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni maofisa wa NBC na viongozi wa kitengo hicho cha gofu.


Nahodha wa Kitengo cha Gofu ya Wanawake cha Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam, Vivienne Mwaulambo (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya maofisa wa NBC baada ya kupokea msaada msaada huo kutoka benki ya NBC. Kutoka kushoto ni, Arden Kitomari, Meneja Chapa na Matangazo, Eddie Mhina; Mshauri wa Mawasiliano na Meneja Udhamini na Matukio wa NBC,Bi. Rachel Remona Kimambo.
SOURCE:PETER MGONGO
Director
Mgongo's Photography and Promotions Co Ltd.
PO.BOX 11452

Dar Es Salaam

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.