Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr .Christina Ishengoma akihutubia katika maadhimisho ya miaka 44 ya St .Egidio Tanzania ,sherehe zilizofanyika Gangilonga mjini Iringa leo
Paroko wa Ismani Angelo Bugro
Mmoja kati ya watu wanaoishi na VVU akitoa ushuhuda wake leo
Mkuu wa mkoa na wageni waalikwa wakiwa na wafanyakazi wa kituo cha Dream leo
wimbo maalum kwa mgeni rasimi mkuu wa mkoa wa Iringa
Wanachama wa Dream ambao wanapatiwa dawa za ARVS na chakula
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christina Ishengoma leo ameshiriki katika maadhimisho ya miaka 44 ya kuanzishwa kwa jumuiya ya st Egidio kupitia mradi wake wa Dream huku akiitaka jamii kuacha tabia ya kuita UKIMWI ni ugonjwa wa masikini .
Akizungumza katika Sherehe hizo zilizofanyika katika viwanja vya Dream katika kata ya Gangilonga mjini Iringa mkuu huyo wa mkoa aliwataka wakazi wa mkoa wa Iringa kuendelea kujitokeza kupima afya zao ili kuweza kunufaika na mpango wa serikali wa kuwasaidia dawa za ARVs kwa wale watakaokutwa na maambukizi ya VVU.
Mkuu huyo wa mkoa amepongeza pia mango huyo wa Dream kwa kazi nzuri ya upimaji wa VVU katika mkoa wa Iringa na kuwa kuanzishwa kwa kituo hicho katika mji wa Iringa ni sehemu ya ukombozi kwa wananchi wa mkoa wa Iringa kujua afya zao .
Hata hivyo ameionya jamii kuepuka kufikiri kuwa UKIMWI ni ungonjwa wa masikini na kuwa hiyo ni dhana potofu ambayo inapaswa kupigwa vita bali ugonjwa huo wa UKIMWI ni ugonjwa wa kila mmoja bila kuangalia uwezo wa kipato
katika risala kituo cha Dream Tanzania iliyosomwa na James Urasa alisema kuwa tok a kituo hicho kimeanzishwa ni mwaka 2010 jumla ya watu 4110 wamepimwa afya zao Kati ya hao watu 2434 hawakukutwa ya VVU na watu 1173 Ndio waliokutwa na maambukizi ya VVU ambapo ni saw a na asalimia 28.5

Na Francis Godwin
No comments:
Post a Comment
Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.