Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Wednesday, February 22, 2012

Majeshi 5,700 zaidi kupelekwa Somalia.

 Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupiga kura ya kuidhinisha jeshi la kulinda usalama nchini Somallia kuongezwa kwa zaidi ya wanajeshi elfu tano.
Wanajeshi hawa wa Kenya kujiunga na AMISOM
Hii itafikisha idadi ya wanajeshi wote wa kuhifadhi amani walio Somalia kufikia 17,731. Kwa wakati huu kuna wanajeshi elfu kumi na mbili wa kigeni nchini humo.
Kura hiyo ya Baraza la Usalama kutaipa fursa jeshi la Kenya ambalo kwa sasa liko nchini Somalia likipambana na Al shabaab ,nafasi ya kupigana chini ya mwamvuli wa jeshi la Umoja wa Afrika.
Upigaji huo wa kura unakuja siku moja tu kabla ya kuanza kwa mkutano wa kimataifa kuhusu Somalia mjini London.
Katika kura hiyo itakayo pigwa hii leo , biashara ya kuuza makaa ambayo ndio njia kuu ya kundi la Al Shabaab kujipatia pesa, itaharamishwa marufuku.
Kundi hilo la Al Shabaab kwa wakati huu linamiliki sehemu nyingi za kusini mwa Somalia ambayo tangu mwaka wa 1991 zimekuwa hazitawaliwi na serrikali ya Kuu.
Katika kipindi hicho cha karibu miongo miwili, wasomali zaidi ya milioni moja na nusu wamehama nchi kufuatia machafuko yasio malizika.
Mwaka jana wapiganaji wa Al Shabaab walilazimika kuuhama mji wa Mogadishu kufuatia mashambulizi makali kutoka kwa yanayoendeshwa na wanajeshi wa umoja wa Afrika .
Mbali na kuweko majeshi ya Uganda, ya Djibouti na yale ya Burundi ,wanajeshi wa Ethiopia pia wameingia nchini Somalia kupambana na Al Shabaab.
Kwa hiyo mapendekezo ya ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa utayapa majeshi yanayopigana chini ya mwamvuli wa jeshi la Afrika fursa ya kuingia sehemu nyegine za Somalia. Hii lengo la kupunguza na hatimae kuondoa kabisa tisho la Al Shabaab nchini Somalia.
Umoja wa Mataifa kupeleka majeshi 5,700 zaidi Somalia.
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupiga kura ya kuidhinisha jeshi la kulinda usalama nchini Somallia kuongezwa kwa zaidi ya wanajeshi elfu tano.
Hii itafikisha idadi ya wanajeshi wote wa kuhifadhi amani walio Somalia kufikia 17,731. Kwa wakati huu kuna wanajeshi elfu kumi na mbili wa kigeni nchini humo.
Kura hiyo ya Baraza la Usalama kutaipa fursa jeshi la Kenya ambalo kwa sasa liko nchini Somalia likipambana na Al shabaab ,nafasi ya kupigana chini ya mwamvuli wa jeshi la Umoja wa Afrika.
Wanajeshi wa AMISOM wakiwa vitani Somalia
Upigaji huo wa kura unakuja siku moja tu kabla ya kuanza kwa mkutano wa kimataifa kuhusu Somalia mjini London.
Katika kura hiyo itakayo pigwa hii leo , biashara ya kuuza makaa ambayo ndio njia kuu ya kundi la Al Shabaab kujipatia pesa, itaharamishwa marufuku.
Kundi hilo la Al Shabaab kwa wakati huu linamiliki sehemu nyingi za kusini mwa Somalia ambayo tangu mwaka wa 1991 zimekuwa hazitawaliwi na serrikali ya Kuu.
Katika kipindi hicho cha karibu miongo miwili, wasomali zaidi ya milioni moja na nusu wamehama nchi kufuatia machafuko yasio malizika.
Mwaka jana wapiganaji wa Al Shabaab walilazimika kuuhama mji wa Mogadishu kufuatia mashambulizi makali kutoka kwa yanayoendeshwa na wanajeshi wa umoja wa Afrika .
Mbali na kuweko majeshi ya Uganda, ya Djibouti na yale ya Burundi ,wanajeshi wa Ethiopia pia wameingia nchini Somalia kupambana na Al Shabaab.
Kwa hiyo mapendekezo ya ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa utayapa majeshi yanayopigana chini ya mwamvuli wa jeshi la Afrika fursa ya kuingia sehemu nyegine za Somalia. Hii lengo la kupunguza na hatimae kuondoa kabisa tisho la Al Shabaab nchini Somalia.

BBC

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.