Wanaharakati wa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI nchini wamewaonya wenzao ambao wanaishi na virusi vya UKIMWI kuacha kujinyanyapaa wenyewe kwa kujificha baada ya kukutwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI .
Wakizungumza leo katika maadhimisho ya miaka 44 ya kuanzishwa wa jumuiya ya St.Gidion kupitia kituo chake cha Dream kilichopo Gangilonga mjini Iringa wanaharakati hao Mariam Samson kutoka mkoani Arusha na Lukelo Lugalla kutoka mjini Iringa walisema kuwa wao ni miongoni mwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI na kuwa hawakuona sababu ya kujificha kwani kukutwa na virusi vya UKIMWI si mwisho wa maisha .
Hivyo walitaka watu wote wanaoishi na VVU kuwa wawazi kwa familia zao na jamii kwa ujumla na kujitokeza kwenda katika vituo kama Dream na vingine kwa ajili ya kupata dawa za kurefusha maisha .
Kwani walisema kuwa unyanyapaa kwa watu wanaoishi na VVU umekuwa ukifanywa na waathirika wenyewe kwa kujiona wao si chochote mbele ya jamii jambo ambalo linapaswa kukemewa kwa nguvu zote na badala yake waathirika wa UKIMWI kuungana na kujitokeza kuelimisha jamii juu ya UKIMWI na hata kuhamasisha watu wengi zaidi kupima
Kwa upande wake Mariam Samson kutoka Arusha alisema kuwa yeye amekuwa akiishi na VVU kwa zaidi ya miaka mitatu sasa na kuwa pamoja na yeye kuwa ameathirika ila mwenzi wake ni mzima wa afya .
Wakati Lukelo Lugalla akidai kuwa alipogundulika kuwa ameathirika aliieleza familia yake na sasa familia yake anatambua na ndio ambao wakati mwingine wamekuwa wakifika Dream kumchukulia dawa na kuwa kwa sasa afya yake ni nzuri zaidi huku akiitaka jamii kuepuka kufikiri kuwa ARVS ni dawa ya kuponya UKIMWI
Na Francis Godwin
No comments:
Post a Comment
Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.