Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Thursday, February 23, 2012

Maneno Ya Busara Yaliyookoa ndoa yangu-short love story

"Hata kama umelewa jifunze kusema maneno sahihi yanaweza kuokoa nyumba yako, na pombe sio"


 Pombe mbaya sana, ilisababisha mke wangu HELEN  akaniacha, nikamfuata na kuomba msamaha akanisamehe. Lakini siku iliyofuata nililewa tena zaidi ya siku zote.na siku hiyo nilijua akiondoka hatarudi tena.
Siku hiyo nililewa sana kwani ilkuwa ni sherehe ya rafiki yangu Hassan, nilirudi nyumbani nimelewa chakali na wala sikukumbuka kuwa nilirudi saa ngapi na  niliingiaje ndani.
Siku iliyofuata niliamka na hangover  na niliogopa nini kitatokea asubuhi ya siku hiyo kutokana na pombe ya jana. Kwa uoga na wasiwasi nilijua kabisa mke wangu ameniacha kutokana na nilivyolewa jana, nilipoamka sikuamini macho yangu kukuta pembeni yangu kuna glass ya maji na aspirini.nikachukua na kunywa. Nikajisikia vizuri kwa kushangaa niliyoyakuta ikabidi nisimame kuangalia nini kinaendelea katika nyumba yangu, kuona pembeni nikakuta viatu vyangu vimeng’arishwa na nguo zangu za kuvaa zimepigwa pasi vizuri. Ikabidi nitoke na kwenda sebuleni, nilipofika sebuleni nikakuta nyumba ipo safi inang’aa imesafishwa. Sikuamini kwani nilijua naachika, kwani nilijua lazima mke wangu atakuwa na hasira na mimi kwa kulewa jana lakini kwa niliyoyaona niliogopa zaidi. Nikiwa nashangaa, nikaona barua na hapo ndipo nikajua ameamua kuniacha kwa barua sasa; nilipofungua barua nikakuta imeandikwa : “mme wangu samahani kwa kutoka nyumbani mapema nimeenda dukani maramoja, leo nitakupikia msosi mtamu sana. Chai ipo mezani jamani jiachie mwenyewe, love you!” Hapo ndipo nilipoogopa zaidi, nikajihisi makosa makubwa sana na kuanza kutetemeka. Ilibidi niende jikoni na kumkuta mtoto wangu wa kwanza Kelvin anakunywa chai; sikupoteza muda na kumuuliza.


Mimi: Kelvin, mwanangu nini kinaendelea? Jana nililewa sana na nilitegemea mama atakuwa na hasira sana leo na ataniacha, sasa ni nini haya?
 
Kelvin: Baba ni kweli jana ulilewa sana na ulikuja usiku sana. Ulichafua sebule na kuvunja glass; huku ukiongea kama mwendawazimu. Kisha mama akakushika, ili akuvue shati ukapiga kelele: acha acha wewe mwanamke  nasema acha mimi ni mme wa mtu, mke wangu ni mmoja tu Helen, nampenda yeye tu, usitumie njia ya mimi kulewa kunilaghai mimi mjanja, mimi ni mme wa mtu niache.Mama alikuacha,  kisha ukajiendea mwenyewe chumbani kulala.

UJUMBE: Hata kama umelewa jifunze kusema maneno sahihi, yanaweza yakaokoa mapenzi yako. Halafu pombe sio nzuri.
Story  by Geophrey Tenganamba

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.