Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Sunday, January 22, 2012

WAPENDA WAKE ZA WATU MPO?


DEREVA wa pikipiki za kukodi maarufu kama 'bodaboda', Mussa Kimbei (43), ameuawa kikatili kwa kucharangwa mapanga na wananchi baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi na mke mdogo wa mfanyakazi wake.

Inadaiwa kuwa marehemu ambaye ni mkazi wa eneo la Kichangani mjini Mpanda alikuwa pia akimiliki shamba la tumbaku ekari nane na ekari nne za shamba la mahindi katika Kijiji cha Kambanga ambapo aliajiri walinzi na vibarua wanane.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Isuto Mantage, mauaji hayo yalitokea juzi saa tano usiku shambani kwa marehemu katika kitongoji hicho cha Kambanga baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi na mke wa msimamizi wa shamba lake aitwaye Christopher Bonge.

Mantage alisema mbali ya kumuua kikatili kwa kumcharanga vipande vipande kichwa kwa mapanga, wananchi hao walichoma moto vibanda vitatu vya kukaushia tumbaku na kufyeka mashamba yake ya tumbaku na mahindi kisha wakateketeza pikipiki yake kwa moto.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwa masharti ya majina yao kutoandikwa gazetini, baadhi ya madereva wa bodaboda ambao wanadai kuwa marafiki wa karibu wa Kimbei, wanadai kwa muda mrefu Kimbei alikuwa akituhumiwa kufanya mapenzi na wake za wanakijiji hao wa Kambaga.

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.