SIRI NZITO MGOGORO WA KKKT IRINGA ,WACHOCHEZI WALIPONA BAKORA
Nimewasamehe bure wote waliohusika kunichafua
Askofu Dr Mdegella akitoa baraka kwa waumini wa kanisa hilo usharika wa kanisa kuu ,pembeni ni askofu Dr Shayo
Askofu Dr Shayo akiendesha ibada hiyo kwa niaba ya askofu Dr Mdegella
Waumini wa kanisa hilo wakisikiliza kwa makini taarifa ya mgogoro huo ulivyokuwa
SIRI nzito yaibuka sakata la mgogoro mkubwa uliokuwa ukilikabili kanisa hilo na kuwa kama si busara za viongozi wa juu wa kanisa katika kumaliza mgogoro huo uliokuwa ukilikabili kanisa hilo la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa kati ya askofu wake Dr Owdernburg Mdegella na baadhi ya waumini wake bakora zingetembezwa kwa wahusika.
Akitangaza kumalizika kwa mgogoro huo mbele ya waamuni wa kanisa hilo usharika wa kanisa kuu Iringa mjini mapema jumapili iliyopita ,askofu wa kanisa la kilutheri Dayosisi ya Makete Dr Hance Mwakabona ambaye ndio alikuwa msemaji mkuu wa kamati maalum iliyoundwa na askofu mkuu wa kanisa hilo Dr Alex Malasusa .
Kabla ya kamati hiyo maalum iliyoundwa kutoka makao makuu ya kanisa hilo ili kuchunguza kiini cha mgogolo huo kwa kufanya mazungumzo ya na pande zote mbili kutangaza kuumaliza mgogolo huo vijana na kanisa hilo na baadhi ya waaumini ambao walikuwa hawapendezwi na kikundi hicho cha watu wachache kumshambulia askofu wao waliapa kuwachalaza bakora wao huo wachochezi.
Mmoja kati ya vijana ambao walikuwa wamechukizwa na mwenendo wa baadhi ya wazee maarufu katika kanisa hilo kwa kuchapisha vipeperushi vya kumtukana askafu Dr Mdegella alisema kuwa wamevumilia vya kutosha na walikuwa hawapo tayari kuendelea kuwavumiliwa watu hao waliokuwa wakiongozwa na mmoja kati ya wazee maarufu katika kanisa hilo kuona wanaendelea na kampeni zao chafu za kuchafua kanisa .
Alisema kuwa mhusika wa mgogoro huo kati ya askofu wao Dr Mdegella na kanisa hilo anafahamika na kuwa wanachopinga na kuchukia ni hatua ya kutumia vipeperushi kama mambo ya siasa katika kulichafua kanisa ni kufanya wamumini wote wanaoabudu katika kanisa hilo kuonekana hawana maana mbele ya jamii.
“Uvumilivu wetu ulikuwa umefika mwisho kama kamati hii kutoka makao makuu ingeshindwa kumaliza suala hili sisi vijana tungelimaliza kwa kuwaadhibu kwa bakora wahusika wa suala hili ambao walikuwa wakichapisha vipeperushi na kusambaza mitaani”
Alisema kuwa ni vipeperushi vya aibu sana ambavyo watu hao walikuwa wakisambaza na katika vipeperushi hivyo kulikuwa na matusi ya makubwa ya nguoni ambayo hayapaswi kusomwa wala kuwekwa bayana katika chombo chochote cha habari .
Kwani walisema kuwa hata kama waliyoyachapisha katika vipeperushi hivyo yangekuwa na ukweli ama uongo njia sahihi haikuwa hiyo ambayo waliitumia ya kuchapisha vipeperushi hivyo na kuvisambaza mitaani bali walipaswa kutumia njia nzuri za kufikisha ujumbe wao hata kukutana na viongozi wa juu wa kanisa kuliko kulidharirisha kanisa la bwana.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati hiyo askofu Dr Mwakabona katika taarifa yake kwa waumini wa kanisa hilo alisema kuwa kamati hiyo ilikutana na makundi yote na hata wahusika wa suala hilo na kuwahoji kwa siri katika mahojiano yaliyodumu kwa takribani siku mbili na kuishi usiku wa manane.
Alisema kuwa mkuu wa kanisa hilo aliunda kamati hiyo yenye wajumbe zaidi ya wanne akiwemo askofu wa Dr Martine Shayo wa Moshi , Askafu Elisha Buberwa na katibu mkuu wa KKKT Brighton Killewa ili kuweza kuja mkoani Iringa kupata ukweli wa mgogoro huo na kuumaliza ili kazi ya kanisa kuendelea.
Kwani alisema kuwepo kwa mgogoro katika moja ya Dayosisi za KKKT nchini si tu madhara yanakuwepo katika dayosisi hiyo pekee bali ni kwa KKKT nzima na kuwa ndio sababu ya kufika na kumaliza mgogoro huo ili kuuanza mwaka 2012 kwa hali ya upendo na mshikamano zaidi .
Hivyo alisema kuwa kwa sasa mgogoro huo umemalizika na wahusika wote wa mgogoro huo wamesamehewa bure na kuwa maazimio ya kamati hiyo baada ya kupokea maoni kutoka katika pende zote ni kuona kuwa wahusika wanasamehewa na kuwa kwa yale ambayo ni makubwa zaidi yenye vithibiti yanafanyiwa kazi taratibu ili kupata ukweli zaidi .
Kwa upande wake askofu Dr Mgedella alisema kuwa yaliyosambazwa na watu hao katika vyombo mbali mbali vya habari likiwemo gazeti maarufu ya kila wiki linalosambazwa kote nchini ni uongo mtupu na kuwa kwa upande wake amesamehe na kama wataendelea kueneza uongo huo basi atalifikisha mahakamani gazeti hilo na kulitaka kumlipa fidia
Na Francis Godwin
No comments:
Post a Comment
Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.