Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Thursday, January 19, 2012

LIGI KUU YA VODACOM KUANZA JUMAMOSI

Mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza
keshokutwa (Januari 21 mwaka huu) kwa mechi nne. Moro United itaikaribisha Yanga
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Mtibwa Sugar itaoneshana kazi na Oljoro JKT
kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani.
Nayo Toto Africans itakuwa mgeni wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mlandizi mkoani
Pwani na Villa Squad itapambana na Kagera Sugar katika Uwanja wa Azam Chamazi, Dar
es Salaam.
Januari 22 mwaka huu JKT Ruvu na Polisi Dodoma zitapepetana Uwanja wa Azam Chamazi
wakati Januari 22 mwaka huu Dar es Salaam itakuwa na mechi mbili; African Lyon na
Azam (Uwanja wa Azam Chamazi) na Simba na Coastal Union (Uwanja wa Taifa).
Ratiba kwa ajili ya waamuzi na makamishna kwa mechi 35 za mwanzo tayari imeshatoka.
Waamuzi wa kati 16 wameteuliwa kuchezesha mechi hizo huku watatu wakiwa wenye beji
za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Makamishna ni 28 huku watathmini wa waamuzi (referees assessors) wakiwa kwenye mechi
tano. Watathmini hao ni Charles Mchau, Soud Abdi, Emmanuel Chaula, Army Sentimea na
Joseph Mapunda.

HAKI ZA MATANGAZO YA TELEVISHENI

Mpaka sasa hakuna kituo cha televisheni ambacho kimeomba na kushinda tenda ya
kuonesha moja kwa moja (live) mechi za Ligi Kuu ya Vodacom. Kwa upande wa vituo vya
redio, vyote vimepewa haki ya kutangaza moja kwa moja mechi za ligi hiyo kwa
masharti yafuatayo;
Kuitambulisha ligi hiyo kwa jina lake (Ligi Kuu ya Vodacom) wakati wa matangazo hayo
ya moja kwa moja, na pia kuweka matangazo ya mdhamini (Vodacom) wakati wakitangaza
mechi husika. Hata hivyo, vituo vya redio bado vinaruhusiwa kuendelea
kutafuta/kutumia matangazo ya wadhamini wao, lakini ambao si washindani wa
kibiashara wa Vodacom.

MECHI YA TOTO AFRICANS VS AFRICAN LYON
Mechi kati ya Toto Africans na African Lyon ambayo kwa mujibu wa ratiba ilikuwa
ichezwe Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza haitakuwepo, na sasa itapangiwa tarehe
nyingine.
Juzi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilipokea barua kutoka kwa wamiliki
wa Uwanja wa CCM Kirumba ikieleza kuwa Februari 5 mwaka huu uwanja huo utatumika kwa
sherehe za kitaifa za kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), hivyo hautaweza kutumika
kwa Februari 4, 5 na 6 mwaka huu.


Source:Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.