Naibu waziri wa Tamisemi Aggrey Mwanri akiingia chini ya kalavati kuchunguza wizi wa mkandarasi alioufanya katika barabara ya Lusitu baada ya kudaiwa kujenga chini ya kiwango
Mwanri akijiandaa kuingia katika mtaro kuhakiki ujenzi wa barabara Ludewa ,ni viongozi wachache sana wanaofuatilia mambo kama hivi
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe aliyesimama akimtazama naibu waziri Tamisemi Mhe.Mwanri akipima urefu wa barabara iliyochakachuliwa badala ya kuwekwa upana futi 7 imewekwa 6
Hapa akibaini uchakachuaji uliofanywa na mkandarasi katika kuibana barabara hiyo
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akimvuta naibu waziri wa Tamisemi kutoka katika mtaro baada ya kujihakikishia mwenyewe wizi uliofanywa na mkandarasi
Mwanri akijiandaa kuingia katika mtaro kuhakiki ujenzi wa barabara Ludewa ,ni viongozi wachache sana wanaofuatilia mambo kama hivi
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe aliyesimama akimtazama naibu waziri Tamisemi Mhe.Mwanri akipima urefu wa barabara iliyochakachuliwa badala ya kuwekwa upana futi 7 imewekwa 6
Hapa akibaini uchakachuaji uliofanywa na mkandarasi katika kuibana barabara hiyo
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akimvuta naibu waziri wa Tamisemi kutoka katika mtaro baada ya kujihakikishia mwenyewe wizi uliofanywa na mkandarasi
NAIBU waziri wancho ofisi ya waziri mkuu serikali za mitaa na serikali za mikoa (TAMISEMI) Aggrey Mwanri ameibua madudu ya kutisha katika miradi ya ujenzi wa nyumba na barabara za wilaya ya Ludewa mkoa mpya wa Njombe na kuonya viongozi wa Halmashauri hiyo kuwa makini na Wizi wa fedha za serikali unaofanywq katika idara ya ujenzi katika wilaya hiyo ya Ludewa.
Akizungumza na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa baada ya kukagua ujenzi wa nyumba za watumishi wa Halmashauri hiyo ,kabla ya kuwahotubia wananchi wachache katika viwanja via stendi kuu ya Ludewa,Mwanri alisema kuwa pamoja na kuwa wilaya hiyo ya Ludewa bado inakabiliwa na changamoto mbali mbali za kimaendeleo ila bado idara hiyo ya ujenzi katika Halmashauri hiyo inaongoza kwa utendaji mbovu na usimamizi mbaya wa fedha za miradi.
Mwanri ambaye leo alilazimila kuwafuata wananchi wa mji wa Ludewa stendi baada ya uwanjani ambako viongozi wa Ludewa waliandaa mkutano wake kukosa watu,alisema kuwa baada ya Kutembelea miradi ya barabara na nyumba za watumishi katika wilaya hiyo ya Ludewa alibaini kuwepo kwa uchakachuaji mkubwa wa fedha za umma.
Kwani alisema kuwa pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na mbunge wa jumbo hilo la Ludewa Deo Filikunjombe katika kulipigania jimbo hilo na wilaya ya Ludewa ili lisonge mbele kimaendeleo ila bado baadhi ya watumishi wamegeuza wilaya hiyo ni sehemu ya wao kuchuma fedha za miradi na kutumia kujineemesha wao.
Alisema kuwa pamoja kuwa Halmashauri mbali mbali zina mchwa ambao wanatafuna fedha za miradi ila kuwa Ludewa inatisha kuona nyumba na barabara zinajengwa chini ya kiwango wakati mhandisi wa wilaya yupo na anaendelea kutazama bila kuchukua hatua.
Pia alisema kuwa tatizo kubwa na mambo Kwenda holela katika wilaya hiyo hasa katika usimamizi wa miradi ya ujenzi wa miradi ni katakana na mhadisi kutokuwa makini na kushinda ofisini badala ya Kwenda kusimamia miradi hiyo.
Hat a hivyo Mwanri alisema katika ziara yake hiyo alipata Kutembelea barabara ya Lusitu ambayo alidai kuwa mkandarasi aliyejenga amejenga chino ya kiwango kutokana na kufinya mita kutoka mita 7 halali hadi mita Kati ya 6 na 5 na nusu na kuagiza mhandisi wa ujenzi katika wilaya hiyo kumtafutia BOQ na mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akimshukuru naibu waziri huyo Mwanri alisema kuwa naibu waziri huyo amekuwa ni kiongozi wa pekee wa kitaifa kufanya ziara katika wilaya hiyo katika kipindi hike cha masika na kudai. Kuwa iwapo viongozi wote wa kitaifa wataiga mfano wa Mwanri Kutembelea wilaya hiyo masika upo uwezekano wa wilaya hiyo kupiga hatua katika maendeleo.
Alisema kuwa Ziara ya Mwanri katika wilaya ya Ludewa imekuwa ya matumaini makubwa katika wilaya ya Ludewa baada ya kubaini kasoro mbali mbali katika miradi na kuwa iwapo kasoro hizo zitafanyiwa kazi wilaya ya Ludewa itapiga hatua katika maendeleo na kuwa kwa upande wake ataendelea kuwatumikia wananchi hao kwa nguvu zake zote.
MWISHO
Chanzo: francisgodwin.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment
Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.