Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Sunday, January 22, 2012

MATEMBEZI YA HISANI YA SAIDIA MAMA MJAMZITO AJIFUNGUE SALAMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Dk. Mary Nagu  (katikati) akimpongeza mama aliyejifungua salama alipotembelea wodi ya Mama wajawazito  katika hospitali ya Manispaa ya Temeke kabla ya kuongoza matembezi ya hisani ya  Saidia Mama Mjamzito Ajifungue Salama yaliyoandaliwa na Taasisi ya Madaktari wahitimu wa vyuo vikuu Tanzania  (THPI) ambayo yalianzia katika Hospitali ya Manisipaa ya Temeke hadi katika Ofisi za Manisipaa ya Tameke, leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Dk. Mary Nagu  (katikati) akiongoza matembezi ya hisani ya Saidia Mama Mjamzito Ajifungue Salama yaliyoandaliwa na Taasisi ya Madaktari wahitimu wa vyuo vikuu Tanzania  (THPI) ambayo yalianzia katika Hospitali ya Manisipaa ya Temeke hadi katika Ofisi za Manisipaa ya Tameke, leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Washiriki wa matembezi ya hisani ya  Saidia Mama Mjamzito Ajifungue Salama wakielekea  katika Ofisi za Manisipaa ya Temeke, leo jijini Dar es Salaam.

Mjengwablog

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.