Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Tuesday, January 24, 2012

Kibaki awataka Wakenya kuwa watulivu


Rais wa Kenya Mwai Kibaki
RAIS wa Kenya, Mwai Kibaki amewataka raia wote wa nchi hiyo kuwa watulivu hasa baada ya uamuzi wa Mahakama ya Jinai Kimataifa (ICC) kuwatia hatiani wakenya wanne kati ya sita waliyokuwa wakikabiliwa na uhalifu wa kibinadamu.
“Nchi hii yetu tukufu imekuwa na changamoto kubwa,” Mwai Kibaki alisema katika taarifa yake. Kenyatta mtoto wa rais wa kwanza wa Kenya na mtu aliyeorodheshwa kama mmoja wa watu matajiri nchini humo ni miongoni mwa wanaokabiliwa na mashtaka pamoja na Mkuu wa Utumishi wa Umma, Francis Muthaura.
Wawili hao, washirika wa rais, wanashutumiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu, ikiwemo mauaji na mateso. Wengine ni Waziri wa zamani wa Elimu, William Ruto na mwandishi wa habari, Joshua arap Sang wanakabiliwa na mashtaka katika kesi tofauti, kwa kuwa walikuwa wapinzani wa Kibaki wakati wa uchaguzi wa mwaka 2007.
Mahakama ya mjini the Hague iliamua hakuna ushahidi wa kutosha wa kuanzisha kesi dhidi ya maafisa wengine wawili. Zaidi ya watu 1,200 waliuawa katika wiki kadhaa za vurugu na watu takriban 600,000 wakalazimishwa kukimbia makazi yao. Wengi bado wanakaa katika makambi ya muda.
Wagombea wawili wa urais nchini Kenya wana kesi ya kujibu juu ya uhalifu dhidi ya binadamu kufuatia vurugu za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai imeamua.
Naibu Waziri mkuu Uhuru Kenyatta na aliyekuwa Waziri William Ruto wote wanakabiliwa na mashtaka. Ni miongoni mwa wakenya wanne mashuhuri – wote ambao wamekanusha madai hayo – wanaokabiliwa na mashtaka.
-BBC

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.