Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Tuesday, January 24, 2012

GLOBAL AFUNGA NDOA NA MAITI YA MCHUMBA WAKE HUKO THAILAND


Dave akitimiza dhamira kwa kumvisha pete kidoleni.
Dave akiibusu maiti ya aliyekuwa mchumba wake.
MKURUGENZI wa kituo kiumoja cha televisheni nchini Thiland aitwaye Chadil Deffy au Deff  Yingyuen, akitaka kuonyesha upendo wake kwa mchumba wake wa siku nyingi aliyekuwa akiitwa Sarinya au “Anne” Kamsook, aliyefariki karibuni katika ajali ya gari, aliamua kufunga ndoa na maiti yake.
Baada ya kufanya hivyo, alizituma picha za tukio hilo kwenye mtandao wa Facebook na YouTube, kitendo ambacho kiliwashangaza watu wengi duniani.
Ndoa hiyo ya ajabu ilifanyika wakati mmoja na mazishi ya maiti ya bi harusi huko Amphur Muang, jimbo la Surin, nchini Thailand ambapo pia palifanyika mazishi ya mchumba huyo aliyekuwa na umri wa miaka 29 sehemu hiyo hiyo.
Deffy ambaye jina lake la utani ni “Dave” alikutana na Sarinya wakati wanasoma Chuo Kikuu cha Asia Mashariki miaka kumi iliyopita na wakapanga kuoana, lakini mwanamke huyo akafariki Januari 3 mwaka huu.

Wakati wa mazishi hayo, bwana harusi alionekana akiwa amevalia suti nyeusi na akimvisha mchumba wake huyo pete.

Tukio hilo lilishirikiwa na marafiki na jamaa wengi wakiwemo wacheza sinema, waimbaji na wanafunzi wenzao wa chuo kikuu hicho ambao walishiriki kwa kuwapa pongezi na kutoa maua.

GLOBAL PUBLISHERS

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.