Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Monday, January 23, 2012

MAKAMU WA RAIS MKOANI LINDI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na mkewe Mama Zakhia Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovic Mwananzila na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Lindi, wakati akikagua Daraja la Mingumbi baada ya kuzindua daraja hilo lililopo Kilwa, akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya mkoa wa Lindi jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Jengo jipya la Bwalo la Shule ya Sekondari ya wasichana Ilulu, iliyopo Kilwa, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya mkoa wa Lindi jana Januari 22, 2012. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovic Mwananzila.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Chumo Namkamba, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi jana Januari 22, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi, alipozindua Daraja la Mingumbi lililopo Kilwa, wakati akiwa kwenye ziara yake ya Mkoa wa Lindi jana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovic Mwananzila.

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.