Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Saturday, January 14, 2012

Kanisa Katoliki la laani uchaguzi DRC

 Kanisa katoliki linasema matokeo sio ya kweli

 Mkuu wa Kanisa Katoliki DRC Kardinali Laurent Mosengwo siku alipokuwa akianza kazi kwenye sherehe katika uwanja wa mpira mjini kinshasa.Kanisa katoliki ni taasisi yenye nguvu kubwa DRC kwani asilimia 60 hadi 70 ya wakongo ni waumini wa kanisa hilo.
 Joseph Kabila
 Sehemu ya kuhesabia kura

Maaskofu wa kanisa Katoliki wametangaza kuwa hawatambui matokeo ya uchaguzi uliofanyika mwezi Novemba huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wakiongozwa na kadinali Laurent Mosengwo, wamewataka wakuu wa tume ya uchaguzi kujiuzulu baada ya kushindwa kusimamia uchaguzi huo.
hesabu za kuraRais Joseph Kabila alitangazwa mshindi huku mpinzani wake Etienne Tshisekedi akidai yeye ndiye rais.

Maaskofu hao 35 wamekuwa wakikutana mjini Kinshasa kutathmini matokeo ya zoezi hilo ambalo pia kanisa hilo lilikuwa na waangalizi kote nchini humo.

Viongozi hao wa kanisa wamesema jukumu la bunge la kwanza ni kuhakikisha kuwa tume nyengine inayojumuisha mashirika ya kijamii, vyama vyote vya kisiasa na makanisa inabuniwa.

Awali raia wengi nchini humo walitarajia kuwa kanisa hilo litaitisha maandamano kupinga matokeo ya uchaguzi huo lakini maaskofu hao wametaka mazungumzo ya maridhiano yafanyike kati ya wanasiasa.

" Tuna hofu kuwa ikiwa utawala utazidi kupuuza ombi la kufanya mazungumzo huenda nchi ikaingia kwenye matatizo ya kisiasa ambayo yalishuhudiwa katika miaka iliopita" alisema katibu wa kundi hilo la maaskofu, Abbot Leonard Santedi.

Waangalizi wa uchaguzi kutoka mashirika ya kimataifa likiwemo lile la Carter Centre kutoka Marekani, walisema uchaguzi huo ulighubikwa na dosari na ni vigumu kutambua mshindi.

Hata hivyo mahakama kuu nchini humo ilimuidhinisha Rais Kabila kama mshindi.

Rais Kabila mwenyewe alikiri kuwa kulikuwepo na dosari lakini sio kiasi kile mshindi hakuweza kutambulika.
BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.