Wasamaria wema wakimbeba Mazola aliyefariki katika ajali hiyo.
Maiti ya Mazola ikiwa katika gari, kulia ni Jumanne ambaye alijeruhiwa vibaya.
Watu wakiitizama moja ya pikipiki zilizohusika katika tukio hilo.
Polisi waliofika kushughulikia suala hilo.
WAKATI wiki iliyopita Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, alifanya mkutano na madereva wote wa pikipiki za biashara maarufu kwa jina la “Bodaboda” jinsi ya kupambana na ajali za mara kwa mara zinasosababishwa na madereva hao, jana majira ya saa tatu usiku maeneo ya Mji Mpya katika manispaa hii pikipki mbili ziligonga uso kwa uso na kusababishwa dereva mmoja kufariki papo hapo huku mwenzake akiwa ameumia vibaya.
Kabla ya kutokea kwa ajali hiyo mwandishi wa mtandao huu aliwashuhudia vijana hao wakifanya mashindano ya kuendesha pikipiki bila kuwasha taa eneo la soko la Mji Mpya ambapo kitendo hicho kilionekana kuwakera kina mama waliokuwa wanafanya biashara ya samaki wa kukaaanga kwenye soko hilo.
Wakiwa mwendo kasi huku wakiwa wamezima taa za pikipiki zao vijana hao ambao mwandishi wetu aliwafahamu kwa jina mojamoja la Mazola na Jumanne, waligongana uso kwa uso kweye makutano ya barabara za mtaa wa Mahiza ambapo Mazola alikufa papohapo na mwenzake akiwa ameumia vibaya sehemu za kichwani.
Katia hali isiyo ya kawaida baada ya kutokea kwa ajali hiyo kinamama waliokuwa wanauza samaki sokoni hapo walionekana kufurahi baada ya kutokea kwa ajari hiyo.
"Safi sana, hawa kifo wamekitafuta wenyewe huwezi kukimbi za pikiki kwa zaidi ya spidi 80 huku umezima taa. Tuliwakanya waache mchezo huo tukihofia wanaweza kuwagonga watoto zetu lakini wametupuuza. Naona sawa wao kupata ajali kwani wamejitakia wenyewe. Ni fundisho kwa madereva wa bodaboda hapa katika kijiwe cha soko la Mji Mpya," alisikika mama mmoja muuza samaki akisema.
HABARI/PICHA NA DUSTAN SHEKIDELE, GPL, MOROGORO

No comments:
Post a Comment
Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.