Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Friday, January 20, 2012

Kifo cha Sumari chabadilisha kikao cha Kamati Kuu CHADEMA


Jan 20th 2012, 13:57

KUFUATIA kifo cha Mbunge Jeremiah Sumari, Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) kimeamua mkutano wa kawaida wa Kamati Kuu ya chama uliokuwa
ufanyike Zanzibar kuanzia Januari 21, 2012 mpaka Januari 22, 2012, sasa
utafanyika Dar es Salaam.

CHADEMA imefikia uamuzi huo ili kuwezesha viongozi wake wakuu wa chama,
wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dkt. Wilbrod Slaa
kuwa karibu ili kujumuika na kuifariji familia ya marehemu pamoja na
kushiriki katika kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu Sumari.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Jeremiah Sumari, mahali pema peponi, Amina.

*Imetolewa leo Januari 20, 2012*
*John Mnyika (Mb), *
*Mkurugenzi wa Habari na Uenezi*

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.