Rais Jakaya Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Joel Bendera wakimaliza kuvuka daraja jipya la Magogoni katika barabara ya Kiganila-Mvuha, Morogoro Kusini mara baada ya Rais Kikwete kulizindua jana.
Rais Jakaya Kikwete akiongea baada ya kuzindua daraja la mto Mtombozi tarafa ya Matombo wilaya ya Morogoro kusini jana.
Rais Jakaya Kikwete mwenye mwamvuli mkononi akielekea jukwaani kuhutubia wananchi huku mvua ikinyesha baada ya kuweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa soko la kijiji cha Mtamba, Morogoro na baadae kuzindua madaraja mawili makubwa katika mto Mtombozi, Matombo, na mto Magogoni katika barabara ya Kiganila-Mvuha na kukagua ujenzi wa barabara sehemu ya Kisaki, Msalabani.
Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akihutubia huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha.
Wananchi wenye mapenzi na Rais wao walikubali kunyeshewa na mvua ili mradi kumsikiliza nini rais kawafanyia na nini anawahakikishia wananchi wake.
Chanzo: magangaone
No comments:
Post a Comment
Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.