Machali ameyasema hayo jana katika mkutano wa NCCR Mageuzi uliofanyika katika uwanja wa Sahara jijini Mwanza uliokuwa na lengo la kuimarisha chama hicho.
Katibu huyo mwenezi wa NCCR Mageuzi amemtaja David Kafulila kuwa ni 'mpuuzi na kigeugeu' kwani ndiye aliye mshauri Mwenyekiti wa Chama hicho James Mbatia kufungua kesi dhidi ya Mbunge wa jimbo la Kawe Halima Mdee aliyemtolea maneno ya kashfa kipindi cha mchakato wa uchaguzi na ndiye aliye mshutumu Mbatia kwa kufungua kesi hiyo dhidi ya Halima Mdee.
Akithibitisha kuwa Mbatia hakuwa na nia mbaya kufungua kesi kama inavyotajwa na Kafulila, Machali alisema kuwa kabla ya kufungua kesi hiyo Mbatia alimwambia Mdee "ukiniomba radhi na kunisafisha kwenye vyombo vya habari sina tatizo na wewe, Halima Mdee akajibu kuwa ukienda mahakamani nitakwenda kukuvua nguo huko huko.
James Mbatia kwa ushauri wa Kafulila akafungua kesi mahakamani lakini mara baada ya kufungua kesi Kafulila ndiye aliyekuwa wa kwanza kumshutumu Mbatia kufungua kesi dhidi ya mpinzani mwenzake na kumtaja kuwa ni kada wa Chama cha mapinduzi (CCM)"
Katibu huyo mwenezi alisema kuwa Kafulila alishamwambia nia yake ya kuukwaa uenyekiti wa NCCR Mageuzi na kwa kuwa alikuwa na ajenda hiyo alianza kumzushia mambo mbalimbali bwana James Mbatia, jambo la kwanza likiwa ni kumtaka mwenyekiti huyo kujiuzuru kwa kushindwa kukiendeleza chama hali inayokifanya kizidi kudidimia.
"Nikamwambia Bunge la 9 lililoishia mwaka 2010 NCCR ilikuwa haina hata mbunge mmoja bungeni leo tuna wabunge wanne chini ya uongozi wa Mbatia, nao wananchi wa Kigoma wamekuamini kwa kampeni na nguvu za huyo huyo Mbatia"
"NCCR ilikuwa na madiwani 19 nchi nzima leo tuna madiwani zaidi ya 40 je haya siyo maendeleo?" alisema Machali kisha akaongeza...
"Nikamwambia, NCCR ilikuwa ikipata ruzuku ya shilingi milioni 1.2 kwa mwezi lakini leo kutokana na idadi ya madiwani kuongezeka tunapata shilingi milioni 12 kwanini tusiige mfano wa wenzetu CHADEMA kwa sisi wabunge wanne tukafanya kazi ya kuaminika majimbo mbalimbali tukaongeza idadi ya majimbo wewe unaanzisha chokochoko zisizo na tija bali kukivuruga chama?"
"Akaniambia 'Ndugu yangu, kaka yangu machali shida yangu ni Uenyekiti' "
"Nikamwambia uenyekiti hautafutwi hivyo subiri 2013 tutakwenda kwenye uchaguzi wa chama wanachama wakikuamini watakupa nafasi"
"Akaniambia 'Achana na mimi' " na ndipo alipoanza kuwarubuni makamishina mbalimbali akiwaambia kuwa ANATAKA KUFANYA MAPINDUZI NDANI YA CHAMA....
Akizianika nyaraka za Kafulila kuomba msamaha vikaoni.
Mh. Machali aliongeza kuwa zaidi ya mara 20 katika kipindi cha mwaka mzima 2011 chama hicho kimekuwa kwenye vikao kikijadili masuala ya Kafulila na mbunge huyo amekwisha onywa na kukiri mwenyewe kuwa amekosa na hatorudia kukivuruga chama lakini kila kiakao kinachoitishwa kimekuwa kikimzungumzia yeye.. Nyaraka za Kafulila kumuomba msamaha mwenyekiti wake James Mbatia kwenye baadhi ya vikao.
Wananchi wakiperuzi baadhi ya nyaraka zilizoanikwa kwenye hadhara hiyo alizoandika Kafulila kuomba msamaa kupitia vikao mbalimbali vya NCCR Mageuzi.
Hii kali zaidi....!!!!!!!!!!
"Chama kimeshindwa kufanya mambo mengi ya maendeleo kwa wananchi wake kwa kupoteza muda kumjadili mtu mmoja, tumekaa chini na kupima uwepo wake chamani na manufaa iwapo tutamtupa nje ya chama hivyo sote kwa pamoja tukasema TUMECHOKA" alisema kwa msisitizo katibu mwenezi huyo wa NCCR Mageuzi Mh. Moses Machali.
Chanzo: http://gsengo.blogspot.com
No comments:
Post a Comment
Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.