Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Tuesday, January 17, 2012

MBUNGE FILIKUNJOMBE AMPONGEZA NAIBU WAZIRI KUMSAIDIA KUIBUA MADUDU LUDEWA

MBUNGE wa jimbo la Ludewa mkoa mpya wa Njombe Deo Filikunjombe amesema kuwa ufisadi ambao naibu waziri wa TAMISEMI ameuona jana katika miradi ya maendeleo wilayani Ludewa ni matokeo ya kazi yake ambayo allianza baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo Hilo na watumishi wa Halmashauri hiyo walionyesha kumpuuza ila sasa wameumbuka.

Alisema kuwa Kila wakati amekuwa akiwataka watumishi na wakuu wa Idara katika wilaya ya Ludewa kufanya kazi kwa uaminifu na kuepuka kuigeuza wilaya hiyo kuwa shamba la bibi kwa kutafuna fedha za miradi ya maendeleo ila hakuna aliyesikia kilio hicho na sasa wamepatikana baada ya ziara hiyo ya naibu waziri wa Tamiseni Aggrey Mwanri.

Mbunge Filikunjombe alisema katika mikutano Yake mingi na ziara zake za Kutembelea miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo akiwa na baadhi ya wakuu wa Idara alipata kuwaonya kuepuka kujenga miradi chini ya kiwango Kwani kufanya hivyo ni kuwakomoa wananchi wa Ludewa ambao wanategemea miradi hiyo kwa maendeleo yao.

"Nilipata kuwakemea Mara kwa Mara haw a watendaji wa Halmashauri ya Ludewa hawakunisikiliza na kujiona wao ni Sawa na sikio la kufa lisilo sikia dawa ila sasa wamekutana na mkubwa wao ....Mwanri kweli nampongeza naibu waziri huyo wa TAMISEMI kwa kufanya kazi vema ya Kuibua ufisadi mkubwa katika miradi ya maendeleo ....napenda kusema kuwa iwapo mawaziri wote wa JK watafanya ziara za Mara kwa Mara Ludewa haw a mchwa katika miradi ya maendeleo watakwisha"

Kwani alisema wilaya ya Ludewa itaendelea kujengwa na watumishi wenye maadili ya utumishi wa umma na wale walioshindwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma ni vema wakaomba kuhamishwa katika wilaya hiyo na kuwaacha wenye uchungu wa kweli wa kuifanya wilaya hiyo kusonga mbele zaidi.

Mbunge Filikunjombe alisema kuwa utendaji mbovu wa baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Ndio unaochangia kurudisha nyuma maendeleo ya wilaya hiyo ya Ludewa na kuwaonya watumishi wasio waadilifu kujirekebisha na pale wanaposhindwa kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi kwa uadilifu ni vema kuomba uhamisho ama kuachana na utumishi wa umma Kwani kamwe hawezi kuvulimia watumishi wachache wakiendelea kutafuna fedha za wananchi wa Ludewa.

Kwa upande wake Naibu waziri Mwanri alimpongeza mbunge huyo wa Ludewa Filikunjombe kuwa ni mmoja Kati ya wabunge ambao wamekuwa mbele katika kupigania Maendeleo kwemye marimba Yao na kuwa wananchi wa Ludewa wanapaswa Kuendelea kutoa ushirikiano kwa mbunge wao huyo ili kuiwezesha Ludewa kusonga mbele katika maendeleo na Kuahidi kuwa ofisi yake itakuwa mbele kupigania maendeleo ya Ludewa.

waziri Mwanri alisema kuwa sehemu yoyote itakapo jitokeza hoja ya fedha za Ludewa kwa ajili ya maendeleo atahakikisha anatetea kwa nguvu zote ili wilaya hiyo ya Ludewa iweze kusonga mbele zaidi .

Aidha alisema kuwa wizara yake haitakubali kuona fedha za miradi katika wilaya hiyo zinatafunwa na kutaka idara inayoongoza kwa usimamizi mbaya wa fedha za umma kuwa ni idara ya ujenzi na kuwa idara hiyo imeonyesha kuchakachua fedha nyingi za maendeleo.

Chanzo: hakingowi.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.