Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Sunday, January 15, 2012

TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE TWIGA STARS YAIFUNGA NAMIBIA 2-0

Na Maganga One Blog.
TIMU ya soka ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars hivi majuzi ilijiweka kwenye mazingira mazuri ya michuano ya Afrika baada ya kuifunga Namibia mabao 2-0 katika mechi iliyochezwa mjini Windhoek, Namibia.
Habari zinasema kwamba mabao ya Twiga yalifungwa
kipindi cha pili na wachezaji Asha Radid 'Mwalala' na Mwanahamisi Shaluwa.

Twiga sasa inajiandaa kucheza mechi ya marudiano jijini Dar es Salaam wiki mbili zijazo.No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.