Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Tuesday, January 24, 2012

Mrembo Avua Nguo Kortini
Richard Bukos na Makongoro Oging’

ELIZABETH Florian ‘Eliza’, Mkazi Dar es Salaam, wiki iliyopita alihukumiwa kifungo cha miezi sita jela baada ya kukutwa na hatia ya kuvua nguo…
Richard Bukos na Makongoro Oging’
ELIZABETH Florian ‘Eliza’, Mkazi Dar es Salaam, wiki iliyopita alihukumiwa kifungo cha miezi sita jela baada ya kukutwa na hatia ya kuvua nguo mahakamani.
Eliza, alifanya kitendo hicho kama sehemu ya kupinga mashtaka dhidi yake ambayo alisomewa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi, Sokoine Drive, Dar es Salaam.
Mrembo huyo, alisomewa mashtaka ya ukahaba kisha akakiri kosa, alipohukumiwa kulipa faini ya shilingi 20,000, alivua nguo na kubaki mtupu.
Kutokana na kutenda kosa hilo waziwazi, tena mbele yake, Hakimu Mkazi, William Mutaki, alimhukumu kwenda jela miezi sita.
Binti mwingine, Evonia William (anaonekana ukurasa wa kwanza akilia), aliibua hekaheka ya aina yake mahakamani.
Evonia, baada ya kusomewa mashtaka ya ukahaba, alikana kosa, hivyo akatakiwa apate wadhamini.
Hata hivyo, baada ya kukosa wadhamini, aliamriwa kwenda mahabusu Gereza la Segerea, Dar, mpaka Januari 31, mwaka huu.
Kutokana na amri hiyo, Evonia aliangua kilio, hivyo kuibua hekaheka ya aina yake, ingawa askari wa mahakama hiyo walifanikiwa kumtuliza baada ya muda mrefu.

From: Global Publishers

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.