Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Thursday, February 23, 2012

"""WEWE NI ZAIDI YA JINSI ULIVYO"""

Jinsi unavyojiona na kuamini ulivyo ndivyo utakavyofanya maamuzi na kuchukua hatua ya maisha yako kwa kujiangalia hivyo.Binadamu ni kiumbe anayehangaika huku na kule kutaka kuyafikia malengo Fulani duniani, tangu azaliwe mpaka atakapoondoka maisha yake yamekuwa katika mfumo wa kutafuta kuyafikia malengo Fulani lakini kutokana na mazingira, hali, watu, mambo anayoyasikia na kuyasoma na mifumo ya maisha Fulani humfanya akubali maisha Fulani yake kwa mipaka Fulani anayoamini yeye na kujiwekea yeye mwenyewe na si kuwa ndivyo alivyo.

Hivyo basi hujikuta kuwa anayoyaamini na kuyakubali ndiyo hayo anayoyaishi na hubaki kama hivyo. Lakini katika kukubali kwake kuhusu yeye alivyo haimaanishi ndiyo hivyo au ndivyo anavyoweza kwasababu anayoyaishi ni yale anayoyaamini kuhusu yeye na yamekuwa kweli kwake. 

Ukweli ni kwamba binadamu ni zaidi ya mwili wake ni zaidi ya damu yake ni zaidi ya nyama yake na hakuumbwa kuishi kwa kuangalia hivyo na tunapoangalia uwezo wake binadamu hatuangalii ukubwa wa mwili wake, kichwa chake, miguu yake au hata ulemavu wake bali tunaangalia zaidi katika mfumo wake wa akili,vipaji na imani yake kuhusu uelewa wake wa ndani kuhusu yeye mwenyewe. Binadamu yeyote ana nguvu zaidi ya mnyama yeyote duniani lakini si katika mwili kwani ni zaidi ya mwili wake.Fikiri kuhusu mambo aliyoyafanya binadamu duniani kisha jiulize ni kiumbe gani kilichofanya mambo kama binadamu? Hata kama kiumbe hicho kina umbile kubwa kiasi gani lakini ukweli utabaki kuwa binadamu ni kiumbe mwenye mambo makubwa sana ambayo mpaka sasa mengine hayajaonyeshwa bado.Jinsi ulivyo ni kutokana na jinsi ulivyojikubali mwenyewe hivyo na haina maana kwamba huwezi kuwa zaidi ya hivyo. Jinsi Bill gates alivyo ni jinsi alivyojikubali alivyo na haina maana kwamba hawezi kuwa zaidi ya hivyo alivyo.


Wewe ni jinsi ulivyo kutokana na jinsi ulivyojikubali hivyo na utakuwa hivyo hivyo siku zote kama ukiishi na kuamini hivyo.Ni kweli mazingira yana nguvu lakini yana nguvu kwa Yule aliyekubali yawe hivyo na kuwa jinsi alivyo. Maisha yako ni jinsi ulivyojikubali wewe lakini kama ukitambua ukweli kuwa wewe ni zaidi ya jinsi ulivyojikubali ulivyo basi dunia hii itawapata watu kama akina Albert Einstein walioamua kujiona tofauti. Binadamu hakuumbwa kama punda na kuwekewa mipaka ya kutembea ardhini chini siku zote bali kama tai anayeweza kuruka angani juu zaidi au hata kuamua kutembea chini kwa matakwa yake.

Yale unayoamini kuhusu wewe ni kweli kama unaamini huwezi ni kweli, lakini ukiamini tena kuwa unaweza ni kweli pia, ukiamini kuwa wewe ni zaidi ya jinsi ulivyo ni kweli na hata ukiamini tofauti ni kweli pia. Hivyo ni uamuzi wako kukubali kuwa huwezi au kukubali kuwa unaweza na kujaribu kufanya katika kuweza.Binadamu tumeumbwa na maajabu ndani yetu, vipaji,uwezo mkubwa ambao wengi hatujautumia ukafika kileleni bila kujali maisha yako ni ya chini kiasi gani, bila kujali mafanikio yako ni ya kati au ya juu kiasi gani unao uwezo mkubwa sana zaidi ya jinsi ulivyo na hujafika kileleni bado.

Hakuna hata binadamu mmoja duniani ambaye alishawahi kufika kilele cha uwezo wake kimafanikio na zaidi hata kiakilli.Na hakuna binadamu asiye na kitu na asiye na kitu ndani yake ni Yule aliyekubali hivyo. Nasema hivi kila mmoja anaishi chini ya uwezo wake na ndiyo maana ukweli utabaki kuwa ukweli kuwa wewe ni zaidi ya jinsi ulivyo.Mwandishi wa Makala hii ni Geophrey Tenganamba, Mshauri wa biashara,Mwanamapinduzi wa maisha,mhamasishaji,msema chochote kinachojenga na mtunzi wa vitabu vifuatavyo;
Kichwa Chako ni Dhahabu Ya Utajiri,Nguvu Ya Kujitajirisha Ndani Yako na The Richest Goldmine in You.
Kwa huduma tajwa; Piga Simu +255714477218 Email:gtlivemore@gmail.com.

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.