Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Friday, February 10, 2012

WAZIRI MKUU ALIPOZUNGUMZA NA MADAKTARI WALIOGOMA NA WAFIKIA MUAFAKA,AWASIMAMISHA KAZI MGANGA MKUU WA SERIKALI NA KATIBU WA WIZARA YA AFYA


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam Februari 9,2.2012. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lymo, Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Hawa Ghasia na Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Marina Njelekela.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari inayoongoza mgomo wa madaktari, Stephene Ulimboka akiuliza swali wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipozungumza na madaktari na wauguzi wa hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam, Februari 9,2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya madaktari na wauguzi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipozungumza nao kwenye Hospitali ya taifa ya Muhimbili, Februari 9, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari inayoongoza mgomo wa madaktari, Stephene Ulimboka baada ya kuzungumza na madaktari na wauguzi wa hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam, Februari 9,2012
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya madaktari na wauguzi wa hospitali ya taifa ya Muhimbili baada ya kuzungumza nao Februari 9, 2012
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwaaga madaktari mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao


No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.