Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Saturday, February 18, 2012

JK Na DK. Slaa Pamoja Tena CCBRT



Rais Jakaya Kikwete akishiriki katika mazoezi ya viungo kabla ya kuongoza matembezi ya hisani kuchangia   ujenzi wa hospitali ya kinamama matatizo mbalimbali ya uzazi katika hospitali ya CCBRT leo asubuhi jijini Dar es salaam. Matembezi hayo yameanzia katika hoteli ya Golden Tulip na kumalizika katika Hospitali ya CCBRT Mikocheni, matembezi hayo yameandaliwa kwa pamoja na kampuni ya Vodacom Tanzania, Vodafone pamoja na hospitali ya CCBRT Kampeni hiyo inaitwa Find your Moyo.


Rais Kikwete akiongoza matyembezi ya Hisani kuchangia ujenzi wa hospitali ya kinamama ya Baobab iliyo chinio ya CCBRT jijini Dar es salaam. Katika picha kutoka kulia Meya wa Ilala Mh Jerry Silaa, Meya wa Kinondoni Mh Mwenda, Bw Erwin Telemans Mkurugenzi mtendaji wa CCBRT, Rene Meza Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya CCBRT Bw. Wilbroad Slaa na kulia kwa Rais ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hadji Mponda na Mkurugenzi wa Vodafone Foundation Bw. Andrew Dunnet pamoja na Mwamvita Makamba wa Vodacom Tanzania katika matembezi hayo leo asubuhi.
PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.