Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Wednesday, February 22, 2012

Dkt. Bilal Akiwa Nkasi

 Makamu wa Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi jengo la Daharia la Shule ya Sekondari ya wasichana ya Korongwe Beach , iliyopo Wilaya ya Nkasi, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Rukwa na Katavi, jana Februari 21, 2012. Kulia kwake ni mkewe Mama Asha Bilal.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda Mti wa kumbukumbu nje ya  jengo la Daharia la Shule ya Sekondari ya wasichana ya Korongwe Beach , iliyopo Wilaya ya Nkasi, baada ya kuzindua Daharia hilo wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Rukwa na Katavi, jana Februari 21, 2012. Nyuma yake ni  mkewe Mama Asha Bilal na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Eng. Stella Manyanya
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Uwanja wa Korongwe kwa ajili ya kuwahutubia wananchi wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Rukwa na Katavi jana Februari 21, 2012.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akinawa maji ya Kisima cha kupampu yanayovunwa kwa mvua, kilichojengwa katika Kijiji cha Mwamapuli wakati alipokuwa katika ziara yake ya mkoa wa Rukwa na Katavi juzi.
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkazi wa Kijiji cha Mwamapuli, Yacoub Jilala, ambaye ni mlemavu, baada ya kumaliza kuwahutubia wananchi wa kijiji hicho, alipofika kuzindua jengo la Ghara la mazao, akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Rukwa na Katavi, juzi Februari 20, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.