Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Tuesday, February 21, 2012

Siku Dr. Mwakyembe Alipokuwa Kanisani kwa Mchungaji Gwajima Kawe

Dk. Harrison Mwakyembe wa pili kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wabunge, kushoto ni Mbunge wa Same Mashariki Mama Anne Kilango Malecela, Waziri wa Afrika Mashariki Samwel Sitta na Mbunge wa Kahama Bw. JamesLembeli.
Dk Harrison Mwakyembe akishuka katika madhabahu mara baada ya kumalizika kwa ibada hiyo leo.
Mchungaji Maximilian Machumu wa kanisa la Ufufuo na Uzima akiwa katika ibada hiyo leo.

Waziri wa Afrika Mashariki Samwel Sitta akishuka katika madhabahu mara baada ya kumalizika kwa ibada leo.
Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima lilloko Kawe Tanganyika Pakers akimkaribisha Dk Harrison Mwakyembe Mbunge wa Kyela na Naibu Waziri wa Ujenzi katika ibada iliyofanyika leo kwenye kanisa hilo na kuhudhuriwa na Waziri wa Afrika Mashariki mzee Samwel Sitta na baadhi ya wabunge kadhaa, Mzee Samwel Sitta amesema Mwakyembe amekwenda kanisani hapo ili kutoa ushuhuda kuhusu ugonjwa wake kwa ujumla. Dk. Harrison Mwakyembe ametoa ushuhuda akimshukuru mungu kwa kumbariki na kuendelea kumpa nguvu juu ya afya njema, Mwakyembe ambaye alikuwa amevalia kofia na Glovu katika mikono yake, ameongeza kwamba tangu alipokuwa ameondoka kwenda nchini India kwa matibabu Oktoba 9 mwaka jana hakuwahi kuvaa viatu, lakini leo amevaa, hivyo akamshukuru mungu kwa miujiza yake.


Mbunge wa Kahama Bw. James Lembeli kushoto , akizungumza na Dk. Harrison Mwakyembe wakati wa ibada hiyo leo.

Waziri wa Afrika Mashariki Samwel Sitta akiongea katika ibada hiyo na kumkaribisha Dk Harrison Mwakyembe ili kuzungumza machache na waumini wa kanisa hilo na kutoa ushuhuda wake.
Baadhi ya waumini wa kanisa hilo wakitawanyika baada ya kumalizika kwa ibada hiyo leo huko Kawe jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.