Blog yenu ya wananchi yenye habari motomoto za kijamii, Blog yenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha. Wapenzi na wasomaji wetu tunaomba ushirikiano wenu ili kuendeleza Blog yetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Wednesday, February 22, 2012

POLISI WAFANYA MAUAJI YA KINYAMA ASUBUHII SONGEA

Wananchi wa songea asubuhi ya leo walikuwa wanaandamana kushinikiza jeshi la polisi lichukue hatua kudhibiti mauaji yanayotokea kila siku mjini hapa. Katika maandamano hayo polisi walianza kuwashambulia wananchi kwa risasi za moto na mabomu ya machozi. mwandishi wa habari hizi amenusurika kupigwa risasi ambayo imempata mtu aliyekuwa jirani yake, ambaye amepoteza maisha hapo hapo. katika mashambulizi hayo mwandishi ameshuhudi watu wawili wamepigwa risasi na kufa hapo hapo. Mpaka na kwenda mtimboni bado risasi za moto zinarindima.


Mwandishi wa TBC akiwa anajihami na risasi za polisi


Mmoja kati ya waliouawa na polisi
Polisi wakifyatua risasi kwa raia
Dimbwi la damu

Chanzo: http://www.songeayetu.blogspot.com/

2 comments:

  1. Huu ni ukatili..Hao polisi kuanzia RPC wawajibishwe vikali..

    ReplyDelete
  2. inatia uchungu..polisi wanapewa taarifa hawachukui hatua madhubuti...watu wanaandamana kudai ulinzi wao wanawaua..polisi sakeni wauaji wa watu wasio na hatia hao majambazi na sio kuua walalamikaji..HATUITAKI TANZANIA YA AINA HII..

    ReplyDelete

Msomaji wetu hakikisha unaheshimu mila na tamaduni za mwafrika,lugha zenye utata au kumkashifu mtu haitapendeza kuonekana kwenye post.Kumbuka vigezo na masharti ya comments kuzingatiwa.Asanteni sana kwa kuwa nasi kwenye blog yenu.